Samatta awataka chipukizi Bongo kufikiria Ulaya

Muktasari:

Mzee huyo anayejulikana kwa jina la Ally Pazi Samatta, amesema wachezaji hao waepuka kuleta mazoea  ya kazi hiyo na kupelekea kuchukuliwa watu wa kawaida kwenye jamii inayowazunguka wakati ni mchezo unaopendwa duniani.

MZAZI wa straika  wa kimataifa Mbwana Samatta anayekipiga Genk ya Ubeligiji, amewata chipukizi katika ligi ya VPL, kutazama zaidi soka la nje, litakalowasaidia kupevuka kifikra.

Mzee huyo anayejulikana kwa jina la Ally Pazi Samatta, amesema wachezaji hao waepuka kuleta mazoea  ya kazi hiyo na kupelekea kuchukuliwa watu wa kawaida kwenye jamii inayowazunguka wakati ni mchezo unaopendwa duniani.

"Simon Msuva, amekuwa mfano mzuri kwao jinsi alivyokuwa anapata sifa Yanga, lakini akaamua kufanya maamuzi ya busara na kupelekea Watanzania waanze kufuatilia soka la Morocco, ili kumuona staa wao anayekipiga klabu ya  Difaa el Jadidi," anasema.

Anatolea mfano wa straika wa Everton , Wayne Rooney, ambaye zamani alikuwa anaichezea Manchester kuwa alipokuja Tanzania kila mmoja alitamani kupiga naye picha ambapo aliwaambia wanapaswa kuiga ili na wao waonekane wana thamani.

"Mfano mwingine upo kwa Samatta, mwanangu huwezi kufananisha thamani yake alipokuwa Lyon, Simba na Tp Mazembe, inaongezeka kila hatua anayokwenda, waige kwa ajili ya mafanikio ya taifa letu kuwa na vijana ambao wanatamaniwa na nchi jirani," anasema.