Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sadala Lipangile: KenGold bado haijashuka

LIPANGILE Pict

Muktasari:

  • KenGold ambayo awali ilijulikana kama Gipco FC (Geita) inatarajia kushiriki Championship msimu ujao baada ya kushindwa kubaki Ligi Kuu kufuatia matokeo iliyopata kwa kuvuna pointi 16 na kushuka daraja ikiwa na mechi tatu mkononi.

BEKI wa KenGold, Sadala Lipangile amesema pamoja na timu hiyo kushuka daraja, wachezaji hawajashuka daraja badala yake mechi tatu zilizobaki ndizo za kujitafuta ili waendelee kubaki Ligi Kuu msimu ujao.

KenGold ambayo awali ilijulikana kama Gipco FC (Geita) inatarajia kushiriki Championship msimu ujao baada ya kushindwa kubaki Ligi Kuu kufuatia matokeo iliyopata kwa kuvuna pointi 16 na kushuka daraja ikiwa na mechi tatu mkononi.

Akizungumza na Mwanaspoti, Lipangile amesema matokeo hayo si mazuri kwao licha ya mipango yao ya kuibakiza timu Ligi Kuu, hivyo kwa sasa kazi iliyobaki ni ya mchezaji mmoja mmoja kuangalia ubora wake.

Amesema mechi tatu zilizobaki ni za kupambania nafasi ya kubaki Ligi Kuu msimu ujao, akieleza kuwa matokeo ya kushuka daraja hawatayapa nafasi kwenye dakika 270 zilizobaki badala yake ni kuangalia fursa.

“Kwa sasa kilichobaki ni jukumu la kila mchezaji kuonyesha uwezo wake ili kubaki Ligi Kuu, timu ndio imeshuka ila siyo kwa mchezaji, hivyo tutatumia hizi mechi tatu zilizobaki kupambania kubaki Ligi Kuu," amesema Lipangile.

Nyota huyo wa zamani wa KMC, ameongeza kuwa wataanza kupambania nafasi kuanzia mechi ya Jumanne hii dhidi ya Pamba Jiji kabla ya kuwavaa Simba na kuhitimisha msimu dhidi ya Namungo.

Amesema wanaodhani timu hiyo haina cha kupoteza kwenye mechi zilizobaki si sahihi sana kwakuwa wachezaji wanayo malengo yao kwani ndio kazi yao ni kucheza soka na watapambana kutafuta matokeo mazuri.

“Siyo kwamba hatuna cha kupoteza baada ya kushuka daraja, sisi kazi yetu ni mpira hivyo lazima tupambanie nafasi kwenye hizi dakika 270 zilizobaki, tunayo malengo kama wachezaji ili kuendeleza vipaji vyetu,” amesema nyota huyo.