Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kipigo cha 2-1 chaiamsha KMC FC

KMC Pict

Muktasari:

  • KMC ilikumbana na kipigo hicho juzi kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam ikiwa chini ya Mbwana aliyechukua mikoba ya Kally Ongala aliyeachana na timu hiyo baada ya makubaliano ya pande mbili kutokana na mwenendo usioridhisha wa mechi za Ligi hiyo.

KICHAPO cha mabao 2-1 kutoka kwa Simba kimeizindua KMC, ambapo kaimu kocha wa timu hiyo, Adam Mbwana amesema wanayafanyia kazi makosa yaliyowaangusha juzi kwani bado kikosi kina ubora wa kuweza kuhimili vishindo wakati Ligi Kuu ikienda ukingoni.

KMC ilikumbana na kipigo hicho juzi kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam ikiwa chini ya Mbwana aliyechukua mikoba ya Kally Ongala aliyeachana na timu hiyo baada ya makubaliano ya pande mbili kutokana na mwenendo usioridhisha wa mechi za Ligi hiyo.

Uamuzi huo umefanyika baada ya kocha huyo kuitumikia timu hiyo kwa miezi mitano na siku 21 tu tangu alipochukua mikoba ya Abdihamid Moallin ambaye aliachana na timu hiyo na kujiunga na Yanga.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mbwana alisema pamoja na kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Simba kikosi chake kilikuwa imara na kilicheza mchezo mzuri na sasa amerudi kwenye uwanja wa mazoezi kuhakikisha anaondoa upungufu uliojitokeza.

“Hatujapata tulichokuwa tunakitaka lakini wachezaji wamefanya kazi nzuri, naamini kama tutafanyia kazi yaliyotugharimu tutakuwa na matokeo mazuri mbele ya Tabora United,” alisema na kuongeza;

“Huu ni mzunguko wa lala salama timu haitakiwi kuingia na akili ya kuwa bora kuliko mwingine tunatakiwa kumuheshimu mpinzani na kumsoma kabla ya kumkabili hiki ndio tunachokifanya ili kuweza kujiweka kwenye nafasi nzuri.”

Mbwana alisema waliingia na mpango mzuri kuikabili Simba na wanaamini hicho walichokifanya ni muendelezo kuelekea mechi zilizobaki huku akiamini kuwa kikosi kilichopo kina kazi kubwa ya kufanya ili waweze kufikia malengo ya kujiokoa na hatari ya kushuka daraja.

“Tunatakiwa kupata pointi tatu mchezo unaofuata dhidi ya Tabora United ili kuirudisha timu mchezoni wachezaji wanatakiwa kuvuja jasho kwani timu haipo kwenye nafasi nzuri na tunakutana na timu ambazo pia zinazihitaji zaidi pointi tatu.”

KMC katika mechi ambazo ilisimamiwa na Ongala kwenye Ligi Kuu, imeibuka na ushindi mara nne, imetoka sare mara nne na imepoteza mechi saba huku ikifumania nyavu mara 13 na kufungwa mabao 23.

Timu hiyo pia iliondolewa katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho la CRDB baada ya kufungwa bao 1-0 na Singida Black Stars.