Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sababu za Yanga kushindwa kuifunga Mwadui hizi hapa

Kukosekana kwa mshambuliaji, Obrey Chirwa na kutokuwa fiti kwa Amissi Tambwe, kumechangia Yanga kushindwa kupata ushindi katika mchezo wa jana dhidi ya Mwadui FC kutoka Shinyanga.

Katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara, Yanga ilibanwa na wageni wao hao kwa kulazimishwa suluhu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Chirwa raia wa Zambia, amefungiwa mechi tatu kwa utovu wa nidhamu. Tambwe alicheza mchezo huo akitokea katika majeraha na hakuwa fiti, alitolewa dakika ya 50.

Yanga ilimtegemea zaidi Ibrahim Ajibu anayecheza nyuma ya mshambuliaji mmoja katika kikosi hicho.

Ajibu alikosa muunganiko mzuri wa Chirwa na Tambwe, hivyo hakuwa kwenye ubora wake tofauti na ilivyotarajiwa.

Mbali ya kupwaya katika eneo la ushambuliaji, Yanga ilicheza taratibu na kutoa nafasi kwa Mwadui kutawala muda mrefu wa mchezo huo.

Yanga iliyoongozwa na Kocha Msaidizi, Shadrack Nsajigwa, baada ya George Lwandamina ambaye hakukaa kwenye benchi, imebaki katika nafasi ya tano ikiwa na pointi 22 na Mwadui imefikisha pointi 13.

Nsajigwa alimtoa Tambwe na kumuingiza Said Mussa, mabadiliko ambayo hayakuzaa matunda licha ya Juma Mahadhi aliyekuwa akicheza pembeni kuingia ndani kucheza nafasi ya Tambwe.

Tangu kuanza msimu huu Yanga imekuwa ikimtumia Chirwa nafasi ya mshambuliaji wa kati na katika mechi alizocheza ameitendea haki kwa kufunga mabao sita akicheza pacha na Ajibu.

Muungano wa Chirwa na Ajibu umezaa mabao 12 baada ya kupangwa katikati akitokea pembeni. Ajibu ni hodari wa kutengeneza mabao akicheza nyuma ya mshambuliaji wa mwisho.

Chirwa ni mahiri wa kufunga akiwa eneo la mwisho la ushambuliaji, ana uwezo kusaidia kukaba katika eneo la kiungo na kuchukua mipira.

Tambwe ana kipaji cha kufunga mabao ya kichwa ni mshambuliaji halisi.

Matokeo hayo yanaiweka Yanga katika mazingira magumu ya kutetea ubingwa na kutoa fursa kwa watani wake wa jadi Simba wakiwa kileleni kwa pointi 26 sawa na Azam.

Mchezo ulivyokuwa

Baada ya kucheza soka ya taratibu muda mrefu, Yanga ilizinduka dakika ya 20 na kufanya shambulizi, lakini Tambwe alishindwa kufunga.

Mwadui ilijibu shambulizi dakika 21 kupitia kwa beki David Luhende aliyeambaa na mpira na kutoa pasi nzuri kwa Paulo Nonga aliyepiga shuti nje. Yanga ilicharuka dakika 25 za mwisho kipindi cha kwanza kwa kufanya mashambulizi mengi kupitia kwa Tambwe, Ajibu na Emmanuel Martin.

Hata hivyo, juhudi zao zilikwaa kisiki mbele ya mabeki wa Mwadui wakiongozwa na Idd Mobby waliokuwa imara kuondoa hatari.

Tambwe alikosa bao dakika ya 33 akiwa katika eneo la hatari baada ya kupata pasi ya Hassani Kessy, lakini alipiga shuti lililookolewa na kipa Anold Masawe.

Dakika ya 37 Yanga ilipata mpira wa faulo baada ya Martin kuangushwa nje kidogo ya 18 na Ajibu alipiga mpira huo kwa ustadi uliogonga mwamba na kutoka nje.

Yanga ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Said Juma ‘Makapu’, Tambwe na Mahadhi na kuwaingiza Said Mussa, Raphael Daud na Yohana Nkomola ambao hakubadili matokeo ya mchezo.

Mwadui iliwatoa Jean GirukishakI, Morris Malaki na kuwaingiza Athumani Rajabu na Morris Malaki.

Kauli ya Nsajigwa

Nsajigwa alisema walijiandaa kupata pointi tatu, lakini Mwadui walisimama kidete licha ya wachezaji wake kucheza kwa juhudi dakika zote 90.

Msikie kocha Mwadui

Kocha wa Mwadui Ally Bizimungu, alisema siri ya kupata suluhu imetokana na kazi nzuri ya wachezaji wake kufuata maelekeo ya benchi la ufundi.