Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rupia akitoka, Mkongomani anaingia Singida BS

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo mwenye mabao 22 katika Ligi Kuu ya DR Congo, ni miongoni mwa nyota wanaopigiwa hesabu ambapo Meneja Mkuu wa Singida, Mkongomani Papy Kimoto ndiye aliyempendekeza ndani ya kikosi msimu ujao.

SINGIDA Black Stars imeanza mchakato wa kusuka upya safu ya ushambuliaji ambapo kwa sasa inafanya mazungumzo na mshambuliaji Candidat Mapendo wa AS Dauphins Noirs ya DR Congo.

Mshambuliaji huyo mwenye mabao 22 katika Ligi Kuu ya DR Congo, ni miongoni mwa nyota wanaopigiwa hesabu ambapo Meneja Mkuu wa Singida, Mkongomani Papy Kimoto ndiye aliyempendekeza ndani ya kikosi msimu ujao.

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Singida zinaeleza mabosi wa timu hiyo wameanza mchakato huo mapema ili kuipata saini ya nyota huyo, huku ikielezwa ni mbadala sahihi wa Mkenya, Elvis Rupia anayeweza kuondoka mwishoni wa 2025-2026.

Rupia aliyejiunga na kikosi hicho tangu kikifahamika Singida Fountain Gate, Septemba 13, 2023, akitokea Kenya Police ya kwao Kenya, inaelezwa huenda akaondoka mwisho wa msimu huu, baada ya kutokuwa na makubaliano ya kuongeza mkataba mpya.

Kutofikiwa kwa makubaliano kati ya uongozi wa Singida na Rupia, kumeanza kufungua mazungumzo ya kumpata mshambuliaji wa AS Dauphins Noirs kutoka DR Congo, Candidat Mapendo ikiwa ni pendekezo la kwanza kwa Kimoto.

Hata hivyo, licha ya Singida kuanza mazungumzo hayo ila hakuna makubaliano rasmi yaliyofikiwa kati ya pande hizo mbili kwa ajili ya kuinasa saini yake, ingawa timu hiyo inapewa kipaumbele cha kwanza kutokana na ukaribu wake na Papy Kimoto.