Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ronaldo, Messi walikacha shule kisa soka

Muktasari:

Messi na Ronaldo hakuna kati yao aliyefurahia masomo au kufanya kazi za shule wakiwa nyumbani baada ya kutoka shule, wakati wote walitafuta namna ya kutoroka ili tu wapate nafasi ya kwenda kucheza mpira na watoto wengine mtaani.

KATIKA toleo lililopita, mwandishi, Luca Caioli alielezea ubinafsi hasa uchoyo wa pasi wa Messi na Ronaldo uwanjani lakini akagusia namna ambavyo wachezaji hao walibadilika na kuwa na rekodi nzuri zilizoonyesha walivyocheza kitimu. Endelea…

Ronaldo pia ni kati ya wachezaji wanaotoa pasi nyingi za kuzalisha mabao katika Ligi Kuu Hispania.

Katika msimu wa 2014/15 pasi zake zilizaa mabao 14, ni idadi kubwa kwa mchezaji wa Real Madrid.

Ni wazi wachezaji wote hao wana ubora katika mtazamo wa kuiangalia timu, wana mchango mkubwa, wamedhihirisha wanaweza kutafuta namna mpya ya kuwa bora zaidi.

Linapokuja suala la mtazamo binafsi wa hulka za mmoja mmoja, Ronaldo na Messi wanatofautiana mno, Messi ni mwenye aibu hataki kuonekana mbele, ni tofauti mno na Ronaldo. Messi ni wa ‘eneo jingine’.

Messi si mtu wa kupenda mambo ya uso kwa uso, jambo ambalo ni tofauti na Ronaldo mwenye umbile la kimaonyesho, ambaye anamvutia kila mtu.

Ni mtu mmoja ambaye anakuwa na wakati mgumu kuendana na eneo fulani dhidi ya mtu wa kujiachia ambaye hajali kutengeneza marafiki, walau huo ndio mwonekano wa mastaa hao kwa haraka haraka.

Ingawa kuna ukweli katika hilo, bado kuna mengi kuliko hali hiyo na ukweli, Ronaldo na Messi wana mengi ya kufanana kuliko hali inavyoweza kuwa katika mtazamo wa haraka haraka. Ukweli, wote wametekwa na hamasa ya kulipenda soka, “Jambo baya ambalo ungeweza kulitumia kumtisha ni kumwambia, huendi kucheza soka leo,” anasema Celia Maria Cuccittini, mama yake Messi.

“Hapana mama tafadhali nitakuwa mtu mzuri na usijali, naahidi.. . acha niende nikacheze,” alikuwa akiomba na kusisitiza hadi ananishawishi.

“Messi hakuwa mtoto mwenye kukasirikasirika na hakuwa mzembe, wakati wote alikuwa kijana mzuri, mkimya na mwenye aibu, ni kama alivyo sasa.”

Messi na Ronaldo hakuna kati yao aliyefurahia masomo au kufanya kazi za shule wakiwa nyumbani baada ya kutoka shule, wakati wote walitafuta namna ya kutoroka ili tu wapate nafasi ya kwenda kucheza mpira na watoto wengine mtaani.

“Aliporudi nyumbani kutoka shule, nilikuwa nikimwambia aende chumbani kwake na kufanya kazi alizopewa shuleni,” anasema mama yake Ronaldo, Dolores.

“Wakati wote alikuwa akiniambia hana kazi alizopewa shule, kwa hiyo nilikuwa nikienda jikoni na kuanza kupika chakula na hapo angeenda kujaribu bahari yake, atachukua maziwa au matunda, atapanda dirishani na baadaye kukimbia akiwa na mpira wake mkononi.

“Kuna wakati angekuwa akicheza soka hadi saa tatu na nusu usiku na hapo ni mbali na zile siku ambazo alikacha kwenda shule ili aende akacheze soka.

Tangu katika umri mdogo tabia na mienendo vilikuwa wazi kwenye uwanja wa soka. Ronaldo alikuwa mpambanaji tangu wakati huo, kama kitu kikifanyika tofauti na alivyotaka angehakikisha hilo linajulikana. Hapo aliweza kulia na kuonyesha hasira kirahisi pale mchezaji mwenzake asipompasia mpira au ikitokea mchezaji mwenzake mwingine amekosa bao au pasi imempita au timu yake haikucheza vile ambavyo angetaka.

Hicho ndicho kilichojitokeza katika mechi moja msimu wa 1993/94 timu yake ya Andorinha ilipofungwa mabao 2-0. “Ronaldo alikosa raha kiasi alilia kama mtoto ambaye alinyang’anywa au kuibiwa mdoli au sanamu aliyependa kumchezea,” anasema Rui Santos Rais wa klabu ya Andorinha.

“Kipindi cha pili aliingia uwanjani na kufunga mabao mawili na kuiongoza timu yake kutoka uwanjani na ushindi wa mabao 3-2, hakika hakupenda kushindwa, alitaka kushinda kila wakati na ilipotokea timu ikafungwa alilia,” alisema Santos.

Itaendelea Jumanne ijayo