Ronaldo afanya kufuru anunua gari ghali zaidi duniani
Muktasari:
Gari hiyo ni mchanganyiko wa gari kongwe ya Bugatti Type 57 SC Atlantic, moja ya magari nne yaliyotegenezwa kati ya mwaka 1936 na 1938.
Turin, Italia. Cristiano Ronaldo amenunua gari ya bei ghali zaidi duniani Bugatti La Voiture Noire wenye thamani ya pauni 9.5milioni.
Taarifa zinasema gari hiyo aina ya Bugatti ilitambulishwa kwa mara ya kwanza duniani katika maonyesho ya magari ya Geneva Motor Show 2019.
Kampuni hiyo ya Kifaransa inayosifika kwa kutegeneza magari ya anasa wameamua kutegeneza gari hilo katika sherehe za kuanzimisha miaka 110 tangu kuanzishwa kwao.
Gari hiyo ni mchanganyiko wa gari kongwe ya Bugatti Type 57 SC Atlantic, moja ya magari nne yaliyotegenezwa kati ya mwaka 1936 na 1938.
Gari hiyo ina 8.0-litre turbocharged W16 engine na uwezo wa kukimbia 260mph.
Bugatti wamethibisha kuwa moja ya gari lao limepata mteja, lakini hawakutaja mmiliki wake.
Gazeti la michezo la Marca la Hispania limemtaja mmiliki huyo mpya ni Ronaldo, pamoja na awali kudai kuwa alinunua gari aina ya Ferdinand Piech, kutoka kwa mwenyekiti wa zamani wa Volkswagen Group.
Mmiliki hataweza kulitumia gari hilo kwa sasa hadi pale 2021 kwa sababu kampuni bado kuna vitu vidogo vidogo wanamalizia kwa mujibu wa taarifa.
Ronaldo ni mpenzi wa magari ya anasa akiwa anamiliki gari aina ya Mercedes C Class Sport Coupe, a Rolls-Royce Phantom, a Ujn Ferrari 599 GTO, a Lamborghini Aventador LP700-4, an Aston Martin DB9, a McLaren MP4 12C pamoja na Bentley Continental GTC Speed.