Rangi ya jezi za Simba Tanzania ni kijivu siyo pinki

Muktasari:
Naona wameanza kujitetea mapema wanajua fika muziki wa Simba msimu ujao ndio maana wanitafuta sababu kila kunapokucha
Dar es Salaam.Mwanachama wa Simba katika tawi la Simba Kasi, Christopher Kabalika amewashangaa wanaowaponda katika mitandao ya kijamii kwamba wamechemka katika kuchagua rangi watakazozitumia msimu ujao kuwa na rangi ya pinki.
Alisema Yanga wana roho ya wivu baada ya kuona jezi zao zimekaa kama brauzi akidai rangi ya Simba ni yakijivu na siyo pinki kama wanavyodai wao.
"Jamani jamani mashabiki wa Yanga, mnajua kweli rangi Simba hii ni ya kijivu, ujue nawashangaa kila wanapokuwa wanasema, wao jezi zimeisha kwa kuwa hawakuwa na pesa za kutengeneza za kutosha.
"Naona wameanza kujitetea mapema wanajua fika muziki wa Simba msimu ujao ndio maana wanitafuta sababu kila kunapokucha, nawaonea huruma watapata tabu sana msimu ujao, hii ndio Simba levo nyingine wakiiga watakufa.
"Nimesikia wanasema wamejaza uwanja, wamshukuru sana Haji Manara anawasaidia sana kuwaamsha akili zao, isingekuwa maneno ya karaha aliyowapa wala wasingekuwa wengi na ndio maana muda wote walikuwa wanatoa vijembe kwani ametawala akili zao, poleni watani wangu Yanga, mpira sio vita ni urafiki," alisema.