Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais wa shirikisho la kuogelea Dunia, Afrika kutua Tanzania

Dar es Salaam. Rais wa Shirikisho la mchezo wa kuogelea duniani (FINA), Husain Al Musallam atawasili nchini Jumatatu akiambatana na maofisa wengine wa ngazi za juu na rais wa Afrika wa mchezo huo, Sam Ramasamy.
Ramasamy pia ni makamu rais wa FINA mbali yakuwa rais wa Afrika wa shirikisho la mchezo huo (CANA).
Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Kuogelea Tanzania (TSA), Asmah Hilal alisema kuwa mbali na viongozi wakuu hao pia kutakuwa na rais wa kanda ya tatu wa CANA, Donald Rukare  pamoja na Brent John Nowicki ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa FINA.
Asmah alisema kuwa katika msafara huo wenye watu tisa, pia atakuwepo Chaykh Ahmad Al Saab ambaye msaidizi wa rais wa FINA, Alex Szanto (FINA jumbe), Mikolaus Schonfeldt (msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa FINA) na bingwa wa zamani wa Olimpiki Ferry Weertam na Ranom Kromowidjojo ambaye ni bingwa wa zamani wa dunia na Olimpiki.
Alisema kuwa ujio wa uongpzi wa juu wa shirikisho la kimataifa na Afrika ni heshima kubwa kwa Tanzania kwani ni mara ya kwanza kihistoria.
Asmah alisema kuwa haijawahi kutokea ujumbe mkubwa wa FINA kutembelea Tanzania tokea nchi ipate Uhuru mwaka 1961 na kuwaomba wadau wa mchezo wa kuogelea kujitokeza kwa wingi katika shughuli mbalimbali za viongozi hao wakuu.
Alifafanua kuwa mara watakapo wasili nchini (Jumatatu mchana), watakwenda moja kwa moja kuangalia mazoezi ya waogeleaji kwenye bwawa la kuogelea la Champion Rise na baadaye kukutana na wadau wa mchezo huo na viongozi wa serikali, Kamati ya Olimpiki na TSA kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Alisema kuwa baada ya kikao hicho cha masaa takribani mawili, viongozi hao watapumzika na kesho yake kuelekea Zanzibar ambapo watakutana na Rais  Dk Hussein Ali Mwinyi.
“Ni faraja kubwa sana kutembelewa na viongozi wa juu wa mchezo wa kugelea duniani. Tunatarajia kuona matunda mazuri ya mchezo huu,” alisema Asmah.