Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Polisi Tanzania gusa unate

Muktasari:

Hata hivyo, Mwanaspoti limenasa mipango kazi ya timu hiyo inayopewa sapoti kubwa na IGP Simon Sirro, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, kwa kusimamiwa na Mwenyekiti, Charles Mkumbo, Robert Munis (Makamu Mwenyekiti), na Frank Lukwaro Kaimu katibu Mkuu.

TIMU ya Polisi Tanzania ndio kioo cha Kanda ya Kaskazini kwa sasa baada ya kushuka kwa JTK Oljoro msimu wa mwaka 2013/14 sambamba na Ashanti United na Rhino Rangers iliyoburuza mkia na sasa inateseka huko Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na msimu uliopita ilimaliza ligi ikiwa nafasi ya saba na kumwacha Polisi ikipanda TPL.

Kupanda kwa Polisi kumeongeza hamasa ya mashabiki kwenye mkoa huo (Kilimanjaro) ambao haijafainika na Ligi Kuu tangu enzi za Timu ya Ushirika ilipokuwa Ligi Daraja la Kwanza (sasa Ligi Kuu), mambo yakaenda kombo na timu hiyo kupotea.

Hata hivyo, Mwanaspoti limenasa mipango kazi ya timu hiyo inayopewa sapoti kubwa na IGP Simon Sirro, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, kwa kusimamiwa na Mwenyekiti, Charles Mkumbo, Robert Munis (Makamu Mwenyekiti), na Frank Lukwaro Kaimu katibu Mkuu.

UONGOZI KICHEKO

“Mipango ipo vizuri na imeanzia kwenye ‘pre Season’ ambapo tumefanya michezo mingi ya kirafiki kwa mafanikio makubwa na kwakuzingatia ripoti ya Mwalimu, lengo kuu ni kuhakikisha tunaleta ushindani ili tuwe katika nafasi za juu ambazo zitatufanya tuweze kuliwakilisha taifa kimataifa.

“Tutahakikisha tunakuwa timu bora kwa kufuata taratibu na miiko ya uendeshaji wa klabu ikiwemo kuhakikisha maslahi ya wachezaji wetu, kikubwa ni kuhakikisha kila mchezaji anakuwa na moyo wa kujituma katika kuhakikisha timu inapata ushindi na anaijua thamani ya nembo kubwa ta Polisi Tanzania FC

“Mashabiki wananafasi kubwa na kupitia timu hii tutawaunganisha mashabiki na washabiki wetu kote nchini na kwa sasa tunawakaribisha hususani wa mikoa ya Jirani ambayo haina timu za Ligi Kuu kama ya Arusha na Manyara,” alisema Frank Lukwaro ambaye ni kaimu katibu mkuu na ofisa habari na mawasiliano wa timu hiyo.

WAPATA MDHAMINI

Ni timu chache ambazo hadi sasa zimefanikiwa kupata udhamini na kuwa na uhakika wa maisha bora kwenye Ligi Kuu msimu huu, Polisi nayo ni miongoni waliofanikiwa kushawishi wadau na kuwekeza ndani ya Maafande hao waliopiga kambi katika Chuo cha Polisi Tanzanis (CCP) lilichokuwepo Kilimanjaro.

“Kwa sasa mdhamini mkuu ni kampuni tanzu ya Lodhia inayojihusisha na utengenezaji wa Nondo, Tanki za maji za Tritank, pia ipo Kampuni ya Busega Mazao inayojishughulisha na uuzaji wa mazao mchanganyiko ya nafaka.

“Tunawakaribisha wadhamini na wafadhili wengine ili waweze kuungana nasi katika msimu huu na kwa uhakika hawatajutia kile watakachowekeza katika klabu yetu,” alisema Lukwaro.

JESHI LA KAZI

Baada ya kufanikiwa kupanda Ligi Kuu Bara, uongozi wa Polisi Tanzania FC, Juni 14 mwaka huu ukamsainisha mkataba wa mwaka mmoja, Suleiman Matola kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo aliyeifundisha Lipuli FC msimu uliopita kwa mafanikio makubwa hadi kutinga fainali ya FA kwa kuitoa Yanga.

Mwenyekiti wa timu hiyo, Charles Mkumbo alisema wameamua kumchukua Matola kutokana na kuwa na historia nzuri kwenye soka la Tanzania tangu akiwa mchezaji na hata kwenye nafasi ya ukocha.

Polisi katika kuimarisha benchi la ufundi walimvuta pia Kocha Ali Suleiman Mtuli kuwa Mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo ikiwa ni moja ya kuifanya timu inakuwa na ushindani mkubwa msimu huu kwa kufanya usajili makini.

Wachezaji wanaounda timu hiyo ni Abddalah Kizega, Abubakari Mkiliundi, Adam Shemahonge, Alhaji Chaduo, Andrea Raymond, Athuman Bakari, Christopher Nyakanda, Daba Hamza, Daud Kijavara,

Daudi Elisante, Denis, Cuthbeti Mushi, Emmanuel Expel, Emmanuel Silvanus, Erick Tawete, Hamad Mshamata, Hanaf Abdi, Hussein Nyawili, Ibrahim Miraji, Ijumaa Kwalakwala, James Mhina na Juma Mbwana.

Wengine ni Kalebi George, Kelvin Paul, Mahamudu Said, Mathayo Malusa, Mohamed Mmanga, Obed Walles, Omar Issa, Omar Kidingile, Oscar Tarimo, Patrick Madidi, Ramadhan Makowa, Shaban Said, Shabani Stambuli, Steven Malisa, Yusuph Yusuph, Sixtus Sabilo, Marcel Bonaventure, Pato Ngonyani na Juma Haji.

Edgar Mfumakule ambaye ni mfungaji bora namba mbili FDL msimu uliopita akiwa na mabao 11, Bantu Admin, Saimon Fanuel, Andrew Bulugu, William Lucian, Baraka Gamba, Henerico Kayombo, Mohamed Ali, Ditram Nchimbi, Iddy Mobby, Kurwa Manzi, Mohamedi Salumu, William Samsoni, , Yassin Salumu, Yassin Mustapha, Hassan Maulid, Mohamed Kassim, Abduly Msantu, Green Paul na Erick Okorai.

MICHEZO YA KIRAFIKI

Timu zote baada ya kusajili zimefanya michezo ya kirafiki ilikuweka mambo sawa kwenye kikosi chao, huku watoto hao wa Matola nao hawakulaza damu kwani walijipanga sasa na msimu tena kwa kucheza michezo zaidi ya minne ya kirafiki.

Walilala bao 1-0 dhidi ya Azam FC, kisha kuilaza Ndanda FC kwa bao 1-0, wakatoshana nguvu ya bao 1-1 dhidi ya Namungo FC kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Majaliwa Mjini Ruangwa, mkoani Lindi kisha kuilaza bao 1-0 katika mchezo wa marudiano katika Uwanja wa Ushirika.

Polisi iliifanyia kitu mbaya Yanga kwa kuilaza mabao 2-1 katika uwanja huo wa Ushirika kwa mabao ya Marcel Kaheza kwa mkwaju wa penalti dakika za mwanzo tu wa mchezo na lile la Ditram Nchimbi.

TUJIKUMBUSHE

Polisi ilisubili hadi mchezo wa mwisho dhidi ya Boma FC kwenye Uwanja wa Ushirika ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kujikusanyia Pointi 47 kwa mabao ya Patrick Madadi dakika ya 13 na 34 huku lile la Boma FC iliyokuwa ikisaka nafasi ya kucheza ‘Playoff’ likifungwa dakika ya 89 na Ramadhan Abdalah.

Usindiu huo uliifanya Polisi kupanda TPL pamoja na Namungo kutoak kundi A.

Polisi itaanza kutupa karata yake ya kwanza kwenye Ligi Kuu kwa kukipiga na Coastal Union kesho Jumamosi, kisha kuvaana na Azam FC, na baadaye kuwakaribisha KMC michezo yote akiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Ushirika, huku mchezo wake wa kwanza ugenini atakuwa na shughuli pevu dhidi ya Yanga, Oktoba 2 Uwanja wa Uhuru.