Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Planet, Eagles ngoma mbichi Mwanza

Planet Pict

Muktasari:

  • Fainali hiyo ya kikapu inachezwa kwa timu kucheza michezo mitano (best of five play off), ambapo katika mchezo wa kwanza Planet ilishinda kwa pointi 71-53, huku ule wa pili ikishinda 67-62, ilhali Eagles ikishinda katika fainali ya tatu kwa pointi 63-55.

TIMU ya kikapu ya Eagles imeifunga Planet kwa pointi 63-55 katika fainali ya tatu ya Ligi ya Kikapu Mkoa wa Mwanza (MRBA) iliyofanyika katika Uwanja wa Mirongo mjini humo.

Kwa matokeo hayo Planet inaongoza kwa kushinda michezo 2-1.

Katika fainali ya nne endapo Eagles itashinda tena  matokeo yatakuwa 2-2 na mchezo wa tano utachezwa

huku timu itakayoshinda katika fainali hiyo itakuwa  bingwa kwa ushindi wa michezo 3-2.

Fainali hiyo ya kikapu inachezwa kwa timu kucheza michezo mitano (best of five play off), ambapo katika mchezo wa kwanza Planet ilishinda kwa pointi 71-53, huku ule wa pili ikishinda 67-62, ilhali Eagles ikishinda katika fainali ya tatu kwa pointi 63-55.

Katika fainali ya tatu, Eagles iliongoza kwa pointi 24-11, 16-23, 7-12 na 16-9.