Pilau buku tu kwa Mkapa

Saturday August 06 2022
Pilau PIC
By Daudi Elibahati

WAKATI sherehe za kilele cha 'Wiki ya Mwananchi' ikihitimishwa leo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, wafanyabiashara nao hawako nyuma kutumia fursa kwa mashabiki waliojitokeza.

Mfanyabiashara wa chakula, Najma Abdallah ambaye ni muuzaji wa pilau amesema kwa leo anauza Sh1000 kwa sahani tofauti na bei ya kawaida ya sh 2000 iliyozoeleka mwanzo.

Najma amesema sababu ya kuuza bei hiyo ni kutoa nafasi kwa kila shabiki aliyehudhuria uwanjani hapa kupata huduma hii bila ya changamoto.

"Pilau haina nyama kwa sababu mtu ambaye ananiletea leo hakuweza kufika kwa wakati ila nashukuru muitikio kwa walaji ni mkubwa." amesema.

Najma aliongeza hadi sasa tayari ameuza zaidi ya sufuria mbili huku akiendelea kupika chakula kingine kutokana na uhitaji kuwa mkubwa.

Yanga inahitimisha 'Wiki ya Wananchi' leo ikiwa ni msimu wa nne tangu kuanzishwa kwake huku ikitarajia kucheza mchezo wa kirafiki na mabingwa wa Ligi Kuu ya Uganda, Vipers utakaopigwa saa 1:00 usiku.

Advertisement
Advertisement