Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Phiri, Baleke wapewa siku nne

Muktasari:

  • Simba iliandika barua Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ili mechi hiyo ya raundi ya tatu ya Ligi Kuu Bara ambayo haijapangiwa tarehe ili ichezwe kupunguza viporo lakini baadaye bodi hiyo haikujibu maombi hayo.

BAADA ya kuona mechi ya Simba na Coastal Union ambayo iliombwa ichezwe keshokutwa Ijumaa, mastaa wa timu hiyo wamepewa mapumziko ya siku nne kuanzia jana Jumatano na watarejea kambini Jumapili.

Simba iliandika barua Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ili mechi hiyo ya raundi ya tatu ya Ligi Kuu Bara ambayo haijapangiwa tarehe ili ichezwe kupunguza viporo lakini baadaye bodi hiyo haikujibu maombi hayo.

Awali kupitia Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally alisema wamekubaliwa mechi hiyo ichezwe lakini baadaye makubaliano hayo yaliota mbawa.

Tayari Simba baada ya mechi yao na Dodoma Jiji iliyochezwa Uwanja wa Uhuru, Jumapili na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 juzi Jumatatu timu hiyo iliingia kambini kujiandaa na mechi yao na Wagosi wa Kaya ambapo jana baada ya bodi kusisitiza ratiba kutokuwa na mabadiliko yoyote kocha Robertinho aliamua kuwapa mapumziko wachezaji wao.

Mwanaspoti lilizungumza na Afisa Habari wa TPLB, Karim Boimanda ambaye alikiri kupokea barua ya maombi ya Simba lakini kilichopelekea kutofanya mabadiliko ya ratiba yao ya ligi ni kutokana na muingiliano wa mechi ya timu ya Taifa Stars inayotarajia kuchezwa kuanzia Septemba 4 hadi 12 mwaka huu ambapo Stars watacheza na Algeria.

“Ni kweli waliandika barua ya kuomba mechi ichezwe Ijumaa lakini sababu ya mechi hiyo kutopangiwa tarehe ama kutochezwa hiyo Ijumaa waliyoomba Simba ni kutokana na ratiba ya Taifa Stars ambao wana mechi ya kufuzu. Kikawaida kocha wa timu ya taifa anatakiwa aingize timu kambini wiki kama mbili kabla ya mechi.

“Sasa wiki hizi zipo ndani ya ratiba ya Taifa Stars, kikanuni pia ni kwamba timu ikitoa wachezaji watatu kwenda timu ya taifa basi mechi zake zinasogezwa na Simba huenda wakatoa wachezaji hao.

“Hivyo hapa ratiba inatubeba wote ili tuwe salama, bodi na timu, maana kama tungeipangia tarehe hiyo mechi na ikatokea Simba imetoa wachezaji zaidi ya watatu wana uwezo wa kugomea mechi kuwa hawatacheza wachezaji wao wapo timu ya taifa,” alisema na kuongeza;

“Hivyo hadi muda huu ratiba ipo pale pale, Simba wasubiri hadi bodi itakapopanga tarehe ya mechi hiyo, ukiangalia pia Coastal wamewapa mapumziko wachezaji wao.”


Kwa Robertinho kimeeleweka

Mashabiki wa Simba wanachekelea kuanza kwa kufunga kwa mshambuliaji wao Mosses Phiri lakini kocha wa wao amefunguka kilichotokea na jinsi anavyokoshwa na Staa huyo kwasasa. Kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema hatua ya kurejea kwa ubora wa Phiri inatokana na juhudi za mshambuliaji huyo kuanzia mazoezini na ilikuwa ni suala la muda tu.

“Tulikuwa tunamuamini Phiri lakini kuna kiwango chake ambacho tulitaka akirudishe ili afunge kama hivi, kwasasa tunaona anaimarika,”alisema Robertinho ambaye awali alikuwa kwenye presha kubwa ya mashabiki wakitaka Staa huyo apewe namba kwa madai kwamba ana kitu.”

Robertinho alisema kurejea kwa Phiri kutaongeza ushindani eneo lao la mwisho la ushambuliaji kati ya Mzambia huyo na washambuliaji wenzake wengine.

“Unaona tukianza na Baleke (Jean) na akafunga lakini kwenye mechi ya Mtibwa pia Onana (Willy) alifunga na mechi iliyopita Phiri akafunga hii Ina maana ushindani kati yao utaongezeka.

“Timu inaendelea kuimarika muda unavyokwenda tuna kikosi ambacho anayetoka na anayeingia hawapishani sana hatuna muda mrefu tutakuwa kwenye kiwango kikubwa.”