Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Yanga kwenye mechi ya kimkakati dhidi ya Fountain Gate

Muktasari:

  • Mechi nyingine zitakazopigwa leo saa 10:00 za jioni, zitawakutanisha maafande wa JKT Tanzania dhidi ya Tanzania Prisons, huku kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, wenyeji Pamba Jiji ‘TP Lindanda’ itaikaribisha Mtibwa Sugar.

MSAKO wa kusaka pointi tatu katika Ligi Kuu Bara unaendelea tena leo kwa mechi tatu kupigwa huku vinara wa ligi hiyo na mabingwa watetezi Yanga watakuwa wageni wa Fountain Gate kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.

Mechi nyingine zitakazopigwa leo saa 10:00 za jioni, zitawakutanisha maafande wa JKT Tanzania dhidi ya Tanzania Prisons, huku kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, wenyeji Pamba Jiji ‘TP Lindanda’ itaikaribisha Mtibwa Sugar.


FOUNTAIN GATE v YANGA

Yanga inayopambana kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Bara, inaingia katika mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuifunga mabao 2-0, Fountain Gate katika mchezo wa kwanza.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 63, baada ya kushinda mechi 19, sare sita na kupoteza moja, huku Fountain Gate inayoshika nafasi ya 10 na pointi 29, ikishinda nane, sare tano na kupoteza 13, zote zikicheza mechi 26.

Kocha wa Fountain Gate, Fredy Felix ‘Minziro’ alisema licha ya mfululizo wa mechi ngumu kwa timu hiyo ila watacheza kwa nidhamu nzuri ya juu ya kuwaheshimu wapinzani wao, ili kutimiza malengo ya kikosi hicho kuepuka janga la kushuka daraja.

“Malengo yetu ni kuhakikisha tunatoka nafasi zote za hatari kwa maana ya kuondoka kabisa kwenye mechi za Play-Off’, sio rahisi kwa sababu ya gepu dogo la pointi na washindani wetu, hivyo, bado tuna kazi kubwa ya kufanya,” alisema Minziro.

Kwa upande wa Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Abdihamid Moallin alisema gepu la pointi na timu zilizokuwa nyuma yao ni chachu ya kikosi hicho kupambana kutimiza malengo ya kutetea taji hilo, jambo ambalo kila mmoja wao hasa wachezaji wanalijua.

“Mechi zote zilizobaki kwa sasa ni ngumu kwa sababu ya mahitaji ya kila mmoja wetu, tunatambua tutakutana na mazingira ya aina hiyo, ila tumejipanga kuhakikisha malengo tuliyoweka tangu kuanza kwa msimu huu tunayatimiza,” alisema Moallin.


JKT TZ v TZ PRISONS

Kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo Mbweni jijini Dar es Salaam, kutakuwa na vita ya maafande ambapo wenyeji JKT Tanzania iliyochapwa mabao 2-1, dhidi ya Singida Black Stars itaikaribisha Tanzania Prisons iliyoichapa Dodoma Jiji 3-1.

Ushidani wa mechi hiyo unachagizwa na nafasi ya 15 inayoshika Tanzania Prisons na pointi 23, katika msimamo wa Ligi Kuu kwa msimu huu, ambapo kikosi hicho kiko katika hatari kubwa ya kushuka daraja, baada ya KMC FC iliyo mkiani kutangulia.

JKT iliyopo nafasi ya sita na pointi 38, haina presha yoyote kwa sasa tofauti na Prisons, ambayo katika mechi zake 26, ilizocheza imeshinda sita, sare tano na kupoteza 15, ambapo endapo itapoteza leo itakuwa katika hatari ya kushuka zaidi.

Ushindi katika mechi mbili zilizopita kwa Prisons baada ya kuifunga Pamba Jiji, kisha kuichapa Dodoma Jiji, inaifanya kuingia na morali ya juu.


PAMBA JIJI v MTIBWA SUGAR

Mechi nyingine ya leo saa 10:00 jioni ya kuhitimisha raundi ya 27, itapigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini, Mwanza, ambapo wenyeji Pamba Jiji itaikaribisha Mtibwa Sugar, huku timu zote mbili zikikutana zikiwa hazina mwenendo mzuri.

Pamba inayoshika nafasi ya saba na pointi 33, inaingia katika mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kuchapwa raundi ya kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar bao 1-0, likiwa ni la kujifunga la nyota wa kikosi hicho, James Mwashinga Januari 25, 2026.