Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Paraguay yaweka historia mpya

Wachezaji wa Paraguay wakishangilia ushindi baad ya kuitoa timu ya Japan kwa matuta.

*Sasa kuivaa Hispania robo fainali Frank Sanga, Pretoria PARAGUAY wamefanikiwa kutimiza ndoto yao ya kufuzu kwa mara ya kwanza kwenye robo fainali ya Kombe la Dunia baada ya kuichapa Japan kwa penalti 5-3 baada ya kwenda suluhu kwa dakika 120. Lakini pamoja na kuweka rekodi hiyo, itakuwa na kazi nzito itakapokwaana na Hispania ambayo nayo imeingia hatua hiyo baada ya kuitoa Ureno kwa kuifunga bao 1-0 katika mchezo mkali uliopigwa kwenye Uwanja wa Green Point ulioko kwenye mji wa Cape Town. Katika mchezo wa kwanza, beki wa Japan, Yuichi Komano atajilaumu mwenye kwa kupiga penalti nzuri iliyogoga mwamba na kutoka na kuifanya Paraguay kumaliza kazi yake kwa ulaini kabisa. Paraguay walionekana kuwa makini zaidi kwa wachezaji wake Edgar Barreto,Lucas Barrios,Cristian Riveros,Nelson Valdez na Oscar Cardozo kupata penalti zao zote huku wachezaji wa Japan, Yasuhito Endo, Makoto Hasebe, Keisuke Honda wakikwamisha mipira wavuni wakati penalti ya Yuichi Komano iliota mbawa. Kimsingi, Paraguay walitawala mchezo huo, lakini Japan ndiyo waliopata nafasi nyingi za kufunga japokuwa walishindwa kuzitumia. Kiungo Daisuke Matsui alitumia vizuri uzembe wa mabeki wa Paraguay na kupiga shuti la umbali wa mita 25, lililogonga mwamba na kutoka nje dakika ya 22. Mchezo huo ulimalizika suluhu na baada ya dakika 120 ndipo mikwaju ya penalti ikachukua nafasi. Mpambano wa Hispania na Ureno ulikuwa wa kuvutia huku kila upande ukikosa mabao mfululizo. Washambuliaji wa Hispania, Alonso, Busquets, Villa na Torres walikuwa hawatulii na mipira kama walivyokuwa wenzao wakiongozwa na Cristiano Ronaldo, Tiago, Simao na Almeida. Hispania iliyoanza fainali za mwaka huu kwa kusuasua, ilipata bao katika dakika ya 63 kama ilivyokuwa katika fainali ya Euro 2008 kwa kuzikutanisha timu hizo. Bao hilo Iilikuwa hivi, Hispania walianza mpira uliokuwa unaendeshwa na Andres Inietsa ambaye naye alimtolea Xavi naye akamwangalia David Villa upande wa kushoto, lakini shuti lake la kwanza lilipanguliwa na kipa Eduardo na mpira ukamrudia, akapiga tena na mpira kugonga dari la goli, likawa bao kwa Hispania. Hata hivyo katika dakika ya 89, Ureno ilipunguzwa nguvu baada ya Ricardo Costa kuonyeshwa kadi nyekundu na mwamuzi, Hector Baldassi wa Argentina kwa kile kilichoelezwa kumkata, Joan Capdevila.