Pambano la Mandonga laondolewa utangulizi

NAIROBI. Pigano kati ya bondia Mtanzania Karim Mandonga na Mkenya Daniel Wanyonyi halitafungua pazia kwa mabondia Mkenya Rayton Okwiri na Mtanzania Shabani Ndaro kama ilivyopangwa awali katika ukumbi wa KICC usiku leo.

Pigano la Mandonga na Wanyonyi katika kitengo cha Super Middleweight cha raundi 10 litakuwa la mwisho baada ya lile la Okwiri.

Mandonga mtu kazi, mwenye uzani wa kilo 83.5 atavalia uzi wa rangi ya samawati nae Wanyonyi atavalia rangi nyekundu akiwa na kilo 80.2.

Majaji Kwenye pambano hilo la kukata na shoka ni Franklyn Imbenzi , Charles Juma na Leonard Wanga. Mwamuzi wa kati ni Julias Odhiambo.

Kwa upande mwingine Okwiri na Ndora watapigana katika kitengo cha Middleweight cha raundi nane. Ukumbini, Okwiri atavalia rangi nyekundu nae Ndoro atavalia samawati.

Mwamuzi wakati atakuwa George Uthman. Majaji ni pamoja na Julias Odhiambo, Franklyn Imbenzi na Charles Oloo.

Bondia wa Tanzania Mandonga mtu Kazi ni mfano wa jinsi masoko yanavyoweza kufanya bidhaa kutamanika.

Misemo yake ya ubunifu imempa umaarufu zaidi kuliko bondia  Mkenya Wanyonyi ambaye ameshinda mataji mengi zaidi.

Jina la pili la Karim Mandonga ni kujiamini. Je, Wanyo ataondoa imani yake na kujitengenezea jina?