Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Pamba Jiji yaja mjini kimkakati

PAMBA Pict

Muktasari:

  • Wababe hao wa zamani waliorejea katika Ligi Kuu msimu huu baada ya kuisotea kwa miaka 23 tangu iliposhuka daraja mwaka 2001, kwa sasa inajiandaa kuifuata Simba jijini humo kuvaana katika mechi ya kiporo cha ligi hiyo kitakachopigwa Alhamisi, huku benchi la ufundi la timu hiyo, likipiga hesabu kali.

PAMBA Jiji imeshacheza mechi nne za Ligi Kuu jijini Dar es Salaam bila kuonja ushindi, ilianza kutoka suluhu na Azam FC kabla ya kunyooshwa 4-0 na Yanga, kisha ikachezea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa KMC na kuibana JKT Tanzania kwa kutoka nayo pia sululu.

Wababe hao wa zamani waliorejea katika Ligi Kuu msimu huu baada ya kuisotea kwa miaka 23 tangu iliposhuka daraja mwaka 2001, kwa sasa inajiandaa kuifuata Simba jijini humo kuvaana katika mechi ya kiporo cha ligi hiyo kitakachopigwa Alhamisi, huku benchi la ufundi la timu hiyo, likipiga hesabu kali.

Benchi hiyo limepanga mikakati mipya ya kuepuka kupigwa nyingi kwa namna wenyeji wao, Simba walivyo kwa sasa katika mbio za ubingwa wakichuana na watetezi, Yanga.

Katika mechi ya kwanza baina ya timu hizo, Pamba Jiji ilipoteza nyumbani kwa bao 1-0 na inaifuata Simba ikiwa na kiu ya kutaka kulipa kisasi, na pia kuhakikisha inacheza kwa akili ili isikumbane na kipigo cha aibu ugenini na kutibuliwa hesabu ilizonazo za kumaliza pazuri.

Kocha mkuu wa Pamba, Felix Minziro alisema kuwa wanajua ubora wa Simba wamekuja kuhakikisha hawarudii makosa waliyofanya mzunguko wa kwanza na kupata matokeo mazuri yatakayowarudisha kwenye nafasi nzuri ya kubaki Ligi Kuu.

“Tunakwenda kucheza na timu ambayo tunajua ina ubora, hilo tumelichukua lakini wana udhaifu wao kwahiyo tutatumia mazuri yao kuyatengeneza yawe udhaifu. Kama unavyoona tumewahi ili kuondoa uchovu kabla ya kuvaana nao, tunaendelea na mazoezi yetu, tunayafanyia kazi siku mbili hizi,” alisema. Minziro.