Pablo apangua kikosi amrejesha Wawa, ampa kazi Kagere

Friday November 19 2021
kagere pic
By Damian Masyenene

KOCHA mpya wa Simba Pablo Franco amekuja kivingine akipangua kikosi cha mwisho cha timu hiyo kilichocheza mchezo dhidi ya Namungo Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Katika mchezo wa leo ambao ni wa kwanza wa Ligi kwa Mhispania huyo, amemrejesha kikosini beki Pascal Wawa ambaye hajaonekana tangu alipocheza mchezo wa ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana, ambapo amechukua nafasi ya Kennedy Juma.

Pia Pablo amemuanzisha Mshambuliaji Meddie Kagere akiwa na kazi nzito ya kuipa mabao Simba akichukua nafasi ya John Bocco aliyeanza katika mchezo uliopita.

Wengine walioanzishwa leo na hawakuanza mchezo uliopita dhidi ya Namungo ni Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga na Bernad Morrison.

Nyota hao wamechukua nafasi za Rally Bwalya (majeruhi), Yusuph Mhilu na John Bocco wanaoanzia nje.

Kikosi cha Simba kinachoanza leo ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohamed Hussein, Joash Onyango, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, Mzamiru Yassin, Meddie Kagere, Kibu Denis na Bernad Morrison.

Advertisement

Wachezaji wa akiba ni Beno Kakolanya, Gadiel Michael, Kennedy Juma, Erasto Nyoni, Sadio Kanoute, Duncan Nyoni, John Bocco, Osmane Sakho na Yusuph Mhilu.

Advertisement