Pablo apangua kikosi akipumzisha mastaa

Sunday May 22 2022
Kikosi PIC
By Damian Masyenene

Mwanza. KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco amepangua kikosi chake kitakachoikabili Geita Gold leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba huku akipumzisha baadhi ya wachezaji ikiwa ni ishara ya kuzingatia mchezo wa nusu fainali dhidi ya Yanga utakaochezwa Mei 28.

Pablo amepangia kikosi chake kilichoanza dhidi ya Azam FC Mei 18, ambapo kipa namba moja, Aishi Manula na beki kisiki, Henock Inonga waliokuwa sehemu ya mchezo huo wakipumzishwa leo dhidi ya Geita Gold.

Beki wa kushoto Mohamed Hussein na Mzamiru Yassin ambao walianza katika mchezo dhidi ya Azam FC leo wameanzia benchi.

Katika kikosi cha leo Pablo ameanza na wachezaji wanne Gadiel Michael, Beno Kakolanya, Paschal Wawa na Thadeo Lwanga ambao hawakuanza katika mchezo uliopita.

Kikosi cha Simba kilichoanza leo ni Beno Kakolanya, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Joash Onyango, Paschal Wawa, Thadeo Lwanga, Kibu Denis, Sadio Kanoute, John Bocco, Rally Bwalya na Pape Sakho.

Wachezaji wa akiba ni Ally Salim, Jimmyson Mwanuke, Mohamed Hussein, Kennedy Juma, Erasto Nyoni, Peter Banda, Mzamiru Yasin, Meddie Kagere na Yusuph Mhilu.

Advertisement


Advertisement