Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ozil kabeba timu Kenya, kisa jezi chakavu

Muktasari:

Ozil kwa mara nyingine tena kaizawadia timu hiyo ya vijina chipukizi nchini Kenya na jezi za Arsenal pamoja na daluga za kuchezea kwa kikosi chote kizima.

KIUNGO mshambuliaji wa Arsenal, Mesut Ozil kaishusha tena baraka zake kwa timu mmoja nchini Kenya iliyooonyesha mapenzi makuba kwake.

Ozil kwa mara nyingine tena kaizawadia timu hiyo ya vijina chipukizi nchini Kenya na jezi za Arsenal pamoja na daluga za kuchezea kwa kikosi chote kizima.

Kikosi hicho cha vijana chipukizi wa kati ya miaka 7 na 14, kilipokea jezi hizo kutoka London kila moja ikiwa na jina ya mchezaji na nambari yake mgongoni.

Mwezi uliopita, Ozil aliguswa sana baada ya kutagiwa kwenye picha moja kwenye Twitter nwa mwanandishi Erci Njiru iliyomwonyesha kijana mwenye miaka tisa Lawrence Masira akiwa malishoni huku kavalia t-sheti nyekundu iliyochakaa huku mgongoni akiwan kaandika nambari 10 (nambari ya Ozil) na jina lake kwa kutukia kalamu ya biro.

Picha hiyo ilimgusa sana Ozil kiasi cha kuamua kumtumia jezi yake orijino tena mpya kutoka London.

Sasa baada ya kupokea jezi lake, Ozil aliamua kuizawadia kikosi kizima cha timu anayoichezea Lwarence safari hii akiwatumia jezi kamili na majina zao pamoja na buti.

“Nimepokea simu kibao kutoka kwa watu wanaofuatilia stori hii na kwa kweli mjukuu wangu Masira na wachezaji wenzake wanastahili hivi wanavyovipata kutoka kwa huyo mchezaji wa Arsenal. Kikweli wanampenda sana na kumshabikia” Nyanyake Masira alinukuliwa na runinga ya Citizen.

Kulingana na mwandishi Njiru, baada ya yeye kumtumia Ozil video ya Lawrence na mdogo wake wakipokea jezi alizowatumia mwanzoni, alimsakamtena.

“Baada ya kutuma zile jezi za kwanza isha nikamtumia video wakizipokea, siku chache baadaye alinitafuta tena na kusema angelipenda kutuma jezi zingine zaidi pamoja na buti kwa ajili ya timu anayoichezea Masira” Njiru alieleza. Kwa hatua hiyo, timu hiyo imebadilisha jina ili kumuenzi na sasa inafahamika kama Ozil FC.