Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Opa apaa ufungaji, Simba Queens yaisogelea Yanga Princess

Opah Clement amefunga mabao saba peke yake na kuiongoza Simba Queens kuichapa TSC Queen ya Mwanza mabao 11-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake uliofanyika kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena uliopo Bunju.


Kutokana na mabao hayo, Opah amefikisha mabao 20 na kumfikia aliyekuwa akiongoza kwa muda mrefu msimamo wa wafungaji, Fatuma Mustapha wa JKT Queens mwenye mwenye mabao 20 pia.


Opah amefurahi kufunga hattrick yake ya nne mpaka sasa msimu huu huku akiahidi kuendelea kufunga zaidi.


"Nafurahi kufunga na kuisaidia timu yangu kupata ushindi. Nimefunga hattrick ya nne na naamini nitaendelea kufunga zaidi.

Opah amefunga mabao yake dakika ya 1,  3, 32, 35, 50, 63 na 67 wakati  mengine yamefungwa na Joelle Bukuru dakika ya 30 na 46 , Asha Jafar dakika ya 17 na 86 wakati la kufutia machozi la TSC Queens limefungwa na Khadija Petro dakika ya 90.


Ushindi waipa faida Simba


Ushindi katika mchezo wa leo umeifanya Simba Queens kupunguza pengo la pointi dhidi ya wapinzani wao wakubwa Yanga Princess na hivyo kuisogelea kwa karibu.


Yanga ndio inaongoza ligi ikiwa na pointi 31 hivyo kuizidi Simba pointi mbili baada ya ushindi wa leo kufikisha pointi 29.