Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mechi za ubingwa ZPL kupigwa leo

ZPL Pict

Muktasari:

Endapo Mafunzo itashinda mchezo wa leo itakuwa na nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) lakini ikipoteza itaiweka nafasi hiyo rehani dhidi ya washindani wenzake ikiwemo Muembe Makumbi na Mlandege.

VITA ya kusaka ubingwa wa Ligi Kuu Zanzibar (ZPL) imekaa kimtego huku mechi mbili zitakazochezwa leo Mei 30, 2025 zimebeba nafasi ya timu kujitengenezea nafasi nzuri.

Kwenye Uwanja wa Mao A, Maafande wa Mafunzo watavaana na Muembe Makumbi, huku Mlandege ikitoana jasho na KMKM kwenye Uwanja Mao B, mechi zote zitaanza saa 10 kisiwani Unguja.

Mafunzo inayoongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 54, inahitaji ushindi ili kufikisha 57 zitakazowasogeza karibu kubeba ubingwa na kubakiza michezo miwili dhidi ya Junguni United na Chipukizi zilizopo kwenye mapambano ya kuepuka kushuka daraja msimu huu.

Katika hatua nyingine, ikiwa Mafunzo itapoteza mchezo huu, itaweka hatarini nafasi ya kubeba ubingwa na kutoa nafasi kwa Mlandege yenye pointi 53 ambayo leo inasaka ushindi kwa KMKM, kisha itacheza dhidi ya Kipanga ambayo bado haipo salama kubaki kwenye ligi na New City iliyoshuka daraja.

Vita ya ubingwa bado mbichi kwani mbali na Mafunzo na Mlandege, KVZ nayo ina pointi 53 ikishika nafasi ya tatu ikibakiza michezo mitatu dhidi ya Uhamiaji, Muembe Makumbi na Kipanga.

Muembe Makumbi ikimalizana na Mafunzo leo, itacheza dhidi ya ikiwamo KVZ na Malindi kuhitimisha msimu.

Mpaka sasa timu nne tayari zimeshapanda daraja ambazo ni Polisi SC na New King SC kutoka Unguja na Fufuni FC na Wawi Star za Pemba.

Pia timu tatu zimeshashuka daraja ambazo ni Tekeleza, InterZanzibar na  New City.

Sasa hivi inasubiriwa timu moja kati ya Mwenge SC, Junguni United, Chipukizi United au Kipanga FC ili kukamilisha idadi ya timu nne zinazoshuka daraja.