Okwa atakata Simba ikiibuka na ushindi kwa Mkapa

Okwa atakata Simba ikiibuka na ushindi kwa Mkapa

What you need to know:

  • Kiungo mpya wa Simba, Nelso Okwa amefungua akaunti ya mabao baada ya kuihakikishia timu hiyo ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya St. George ya Ethiopia katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Mkapa.

Kiungo mpya wa Simba, Nelso Okwa amefungua akaunti ya mabao baada ya kuihakikishia timu hiyo ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya St. George ya Ethiopia katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Mkapa.

ILIKUWA ni zaidi ya shoo. Mashabiki wa Simba wameondoka kwa Mkapa kiroho safi kufuatia ushindi wa chama lao kwa mabao 2-0 dhidi ya St. George.

Mabao ya Kibu Dennis na Nelson Okwa yametosha kuhitimisha tamasha la 14 la Simba tangu kuanzishwa kwake, 2009.

Kivutio kikubwa kwa Simba kwenye mchezo huo wa kirafiki ilikuwa ni nyota wao wapya Mohammed Ouattara ambaye alicheza sambamba na Henock Inonga.

Huku wengine ikiwa ni Okwa, Moses Phiri na Dejan Georgijević ambaye alingia kuchukua nafasi ya Habib Kyombo aliyepika bao la kwanza la Simba.

Mbali na wachezaji hao wapya kufanya vizuri kwenye mchezo huo wa kirafiki, mwamba wa Lusaka, Clatous Chama alitikisa baada ya upishi mzuri wa bao la pili la Simba baada ya kuihadaa ngome ya St. George ya Ethiopia.