Ni mwendo wa wachezaji kupishana

WACHEZAJI  wa Ihefu, Kiungo Shaban Msala na mshambuliaji Charles Ilamfya wamejiunga na Mtibwa Sugar baada ya kuvunjiwa mikataba yao.

Wawili hao walikuwa wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Ihefu, lakini ujio wa wachezaji wengine, kumefanya wawili hao kuondoka na kwenda Mtibwa.

Mwanaspoti linafahamu Msala leo usiku alitumiwa mkataba na Mtibwa Sugar kwa ajili ya kuusaini na kuingizwa kwenye mfumo wa usajili, huku Ilamfya, akiwa tayari amesaini mkataba wa miezi sita.

Msala ni kama wamepishana na Kelvin Nashon aliyeondoka Mtibwa na kwenda kujiunga na Ihefu, huyo ndiye anayecheza nafasi yake, wakati Ilamfya kuondoka kwake  Ihefu kampisha  Elvis Rupia aliyetokea Singida Fountain Gate.