Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ngushi aibeba Mashujaa, Coastal Union hoi

Ngushi Pict
Ngushi Pict

Muktasari:

  • Ngushi amefunga bao hilo pekee dakika ya 14 akipokea pasi ya beki Abderhman Mussa, kisha mfungaji kuwatoka kiakili mabeki na kipa bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, Ley Matampi wa Coastal Union.

Bao la mshambuliaji Crispin Ngushi, limetosha kuipa ushindi wa pili Mashujaa, ikiendeleza makali yake kwenye Ligi Kuu Bara ikiwalaza Coastal Union ya Tanga.

Ngushi amefunga bao hilo pekee dakika ya 14 akipokea pasi ya beki Abderhman Mussa, kisha mfungaji kuwatoka kiakili mabeki na kipa bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, Ley Matampi wa Coastal Union.

Ushindi huo unaifanya Mashujaa kupaa hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikifikisha pointisaba kwa kushinda mechi mbili na sare moja.

Kipigo hicho cha Coastal Union kinaifanya timu hiyo kufikisha mechi mbili bila ushindi ikibaki nafasi ya 13 na pointi moja iliyotokana na sare ya bao 1-1 iliyoipata dhidi ya KMC.

Kwenye mchezo huo uliopigwa Uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam Coastal ikiwa mwenyeji  imeonyesha kiwango cha kawaida ikikosa makali kwenye safu ya ushambuliaji.

Ngushi ambaye ametua Mashujaa akitokea Coastal Union, ameendelea kuwa usajili  mzuri kwa Wanajeshi hao akifunga bao la pili msimu huu ambapo kwenye mechi mbili alizofunga timu yake umeibuka na alama tatu.

Licha ya Coastal Union kimrejesha uwanjani beki wake, Lameck Lawi kwenye mechi ya leo, bado ukuta umendelea kuruhusu mabao kwenye mechi ya pili msimu huu.