Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ngumi Taifa yaita 20

Muktasari:

Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema kuanzia leo Jumatatu wanaanza kuwaombea ruksa mabondia hao kwa waajiri wao ili kuweza kuingia kambini chini ya Kocha Mkuu kutoka Kenya, Mussa Benjamini Oyimbo.

SHIRIKISHO la Ngumi Tanzania (BFT) limetangaza kikosi cha mabondia 20, watano kati yao wakiwa ni wawake kwa ajili ya kuunda timu ya taifa itakayojiandaa na michuano ya Afrika itakayofanyika kati ya Mei 25-Juni 4 nchini Congo Brazzaville.
Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema kuanzia leo Jumatatu wanaanza kuwaombea ruksa mabondia hao kwa waajiri wao ili kuweza kuingia kambini chini ya Kocha Mkuu kutoka Kenya, Mussa Benjamini Oyimbo.
Mashaga alisema uteuzi huo umefanywa kupitia michuano ya Taifa iliyomalizika hivi karibuni jijini Dar es Salaam kupitia Kocha Michael Yombayomba na makocha wengine walioteuliwa kuangalia wanaofaa kuichezea timu hiyo ya taifa.
Uteuzi huo unaelezwa umezingatia uwezo wa sasa wa kucheza mchezo wa ngumi, umri unaokubalika kwa mujibu wa Sheria za Shirikisho la Ngumi cha Dunia (AIBA)  na tabia binafsi ndani na nje ya ulingo.
Walioteuliwa katika timu hiyo ni Herman Richard, Ibrahim Abdallah, Ezra Paulo, Ismail Galiatano, King Lucas, Mohammed Juma, Kassim Seleman, Said Ramadhan, Haruna Hussein, Seleman Kidunda, Yusuph Changarawe  na Haruna Swanga.
Wengine ni Mhina Morris, Alex Sitta na mabondia watano wa kike ambao ni; Sara Andrew, Grace Joseph, Siwatu Eliuta, Sarafina James na Aliskunda Jonas.
"Timu hii itaiwakilisha nchi katika mashindano ya Afrika ya Congo na wengine wataenda Uganda katika mashindano ya Afrika Mashariki," alisema Mashaga.