Ngoma ngumu dakika 45 za kwanza za Yanga v Prisons

Dakika 45 za kipindi cha kwanza katika mchezo wa Kombe la FA hatua ya mtoano kati ya wenyeji Prisons dhidi ya Yanga zimekamilika huku hakuna timu iliyofanikiwa kupata bao.
Yanga ndio walioonekana kutulia katika dakika 45 za kwanza wakitengeneza mashambulizi makali ambayo yangeweza kuwapatia mabao.
Yanga waliuanza mchezo kwa kasi na dakika ya kwanza tu almanusura mshambuliaji Said Ntibazonkiza aipatie bao timu yake akishindwa kuunganisha mpira wa kichwa wa beki wake Lamine Moro kufuatia mpira wa kona uliopigwa na Carlos Sterios "Carlinhos'


Shambulizi lingine zuri kwa Yanga
Dakika ya 20 beki Abdallah Shaibu 'Ninja' anaunasa mpira mzuri wa krosi kutoka kwa  Carlinhos lakini kichwa cha kinatoka nje kidogo.

Dakika ya 21 wenyeji Prisons wanafanya shambulizi zuri la haraka mshambuliaji Jeremia Juma anapokea mpira safi ndani ya eneo la hatari anaachia shuti Kali linatoka nje akipokea pasi ya beki wake wa kulia Michael Ismail.
Dakika ya 37 nahodha wa Prisons Benjamin Asukile anapoteza nafasi nzuri akishindwa kuunganisha krosi ya Salum Kimenya.
Yanga wameonekana kutulia wakicheza pasi za uhakika huku katika ulinzi wakionekana kucheza kwa tahadhari kubwa.
Yanga wametengeneza mashambulizi ya hatari zaidi kushinda wenyeji wao lakini shida ipo katika umaliziaji.