Ngai aongoza mazishi Mwenyekiti Baraza la Wazee Yanga
Muktasari:
- Mazishi hayo yaliyohudhuriwa na mamia ya wadau mbalimbali Yanga iliwakilishwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Alexander Ngai na viongozi wengine akiwemo Mkurugenzi wa Mashindano wa klabu hiyo Ibrahim Mohammed.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Yanga Abdulrhman Munelo amezikwa kwenye makaburi ya Mbagala Kingugi.
Mazishi hayo yaliyohudhuriwa na mamia ya wadau mbalimbali Yanga iliwakilishwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Alexander Ngai na viongozi wengine akiwemo Mkurugenzi wa Mashindano wa klabu hiyo Ibrahim Mohammed.
Munelo alifariki juzi kwa ajali ya pikipiki iliyogonga Lori kwa nyuma na kupoteza uhai, tukio lililotokea Mbagala Zakiem.
Akizungumza mara baada ya mazishi hayo Ngai alisema Yanga imepoteza nguzo muhimu kufuatia nguvu ya Munelo katika kuipigania klabu Yao na hata kuwaunganisha wengine.
"Kifo Cha Munelo ni pigo kubwa kwa klabu yetu, mtu mliyekuwa naye siku Moja kabla na baadaye mnasikia amefariki kiukweli imetuumiza kama klabu," alisema Ngai
"Huyu ni Mzee wetu aliyekuwa anayaunganisha makundi mbalimbali ndani ya klabu yetu lakini kubwa tutakalomkumbuka ni namna alivyo tayari kuipigania klabu kwenye lolote aliloweza."