Neymar atupia picha Instagram akiwa na mtoto wa Jackie Chan
Mchezaji wa Barcelona, Neymar anayetajwa kutimkia PSG, amekutana na Jaycee ambaye ni mtoto wa mkali wa filamu, Jackie Chan na kuweka picha kwenye mtandao wake wa Instagram.
Neymar alionekana kufurahia baada ya kukutana na mtoto wa Jackie Chan, huku akimweleza kupeleka salamu kwa baba yake kutokana na kazi kubwa aliyoifanya kwenye tasnia ya filamu.
Mshambulaji huyo alituma picha akiwa amemkumbatia Jaycee huku akiandika; “Ni jambo la furaha kukutana nawe jaycee_chan pia usisahau kumkumbatia baba yako kwa ajili yangu.”