New King yavunja mwiko na kupanda ZPL

Muktasari:
- Timu ya New King yenye historia ya kuishia katika hatua ya pili ya mtoano wa daraja la kwanza imefanikiwa kuvunja ukuta huo leo jioni baada ya kutoka suluhu katika mchezo wa marudio ambapo hatua ya kwanza ilisulubu Sebleni kwa mabao 3-2 na sasa rasmi timu hiyo kucheza ZPL msimu ujao.
Timu ya New King maarufu 'Wachoma Mahindi' imetegua kitendawili kilichokuwa kikiulizwa na wengi kwa miongoni mwa timu zilizopanda daraja na msimu ujao itacheza Ligi Kuu Zanzibar(ZPL).
Timu nyingine zilivuka hatua hiyo kwa Kanda ya Pemba ni Wawi na Fufuni zitakazocheza ZPL kwa kwa mara ya kwanza pia.
Wachoma Mahindi wametinga hatua hiyo baada ya kuitandika mabao 3-2 Sebleni ikiwa ugenini, ushindi ulioipa nafasi ya kupanda Ligi Kuu kwani leo katika marudiano kutoka kwa suluhu wakiwa wenyeji wa mchezo huo.
New King yenye historia ya kuishia katika hatua ya pili ya mtoano wa daraja la kwanza imefanikiwa kuvunja ukuta huo leo jioni na rasmi kucheza ZPL msimu ujao.
Mechi ya jasho na damu itapigwa kesho Jumapili saa 10 jioni katika Uwanja Mao A, utakaowakutanisha Maafande wa Polisi na Kundemba baada ya mchezo wa kwanza kutoka sare ya bao 1-1.
Mashabiki wa soka Zanzibar wanasema kesho dakika 90 za mchezo huo mkali na unaosubiriwa kwa shauku utabainisha nani katika yao watatinga ZPL huku wote wakiwa wanaitaka ligi hiyo.
Polisi na Kundemba zilishuka daraja msimu uliopita.