Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ndumbaro aukagua Uwanja wa CCM Kirumba, kufanyiwa ukarabati kuelekea Afcon 2027

Ndumbaro Pict
Ndumbaro Pict

Muktasari:

  • Dkt. Ndumbaro amefanya ukaguzi huo leo Julai 2, 2024 akiwa ameambatana na Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula ambapo amekagua eneo la kuchezea, vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji, maliwato na eneo la watu mashuhuri.

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro amekagua hali ya Uwanja wa CCM Kirumba uliopo jijini Mwanza ambao upo kwenye mpango wa kufanyiwa ukarabati mkubwa kwa ajili ya mashindano ya Afcon 2027.

Dkt. Ndumbaro amefanya ukaguzi huo leo Julai 2, 2024 akiwa ameambatana na Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula ambapo amekagua eneo la kuchezea, vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji, maliwato na eneo la watu mashuhuri.

Baada ya ukaguzi huo, Dkt. Ndumbaro amesema mpango wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kufanya ukarabati mkubwa wa uwanja huo ambao utatumika kama uwanja wa mazoezi wakati wa michuano hiyo ambayo nchi za Tanzania, Kenya na Uganda zitakuwa mwenyeji.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo, Angelina Mabula ameishukuru Serikali kwa kuujumuisha uwanja huo katika mpango wa AFCON 2027.

Viwanja vingine vitakavyokarabatiwa ni Jamhuri uliopo Morogoro, Majimaji (Songea), Mkwakwani (Tanga) na Sokoine (Mbeya).