Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtibwa Sugar yakomalia mastraika, viungo

MTIBWA Pict

Muktasari:

  • Zoezi hilo la kusaka nyota wapya lilianza Julai 10 na litahitimishwa Julai 14 linafanyika Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro,  chini ya kocha wa timu za vijana, Awadhi Juma ‘Maniche’ aliyesema vijana walijitokeza kwa wingi hasa wale wa U-17.

MTIBWA Sugar iliyorejea Ligi Kuu Bara baada ya kushuka msimu wa 2023-2024, imeanza mchakato wa kusaka vipaji vya vijana wenye umri chini ya miaka 17 na U-20 ili kuboresha vikosi vyao kwa ajili ya msimu ujao lkini wakilenga zaidi eneo la ushambuliaji na kiungo ambako wamebaini linawasumbua.

Zoezi hilo la kusaka nyota wapya lilianza Julai 10 na litahitimishwa Julai 14 linafanyika Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro,  chini ya kocha wa timu za vijana, Awadhi Juma ‘Maniche’ aliyesema vijana walijitokeza kwa wingi hasa wale wa U-17.

Maniche alisema wanachokiangalia kwa wachezaji hao ni vipaji vikubwa watakavyoviendeza, hivyo inakuwa ngumu kwao kutaja idadi.

“Siwezi kutaja ni idadi ya wachezaji wangapi, tunachokiangalia ni vipaji vya wachezaji ambao tukiwaendeleza watafanya makubwa, ila maeneo tunayoyahitaji zaidi ni washambuliaji na viungo,” alisema na kuongeza;

“Katika timu ya vijana wa U-17 tuna wachezaji 30 na U-20 tuna wachezaji 25, tukikamilisha zoezi ndipo tutajua kila timu kwa ajili ya msimu ujao ina wachezaji wangapi.”

Maniche aliyewahi kuwika na Simba na Mtibwa, alisisitiza zoezi hilo linafanyika bure, isipokuwa mchezaji atajigharamia nauli, chakula na sehemu ya kulala kwa muda wote wakati zoezi hilo likifanyika.

“Kumekuwa na malalamiko ya watu kusema Mtibwa tunalipisha pesa ili mchezaji kupata nafasi, vitu hivyo havipo na hao ni matapeli, klabu hii ipo kwa ajili ya kukuza vipaji vya wachezaji,” alisema Maniche.