Ndo hivyo Ronaldo akiondoka Juventus, anatua huku

Muktasari:

Mkataba wa Ronaldo huko Turin unafika tamati 2022, lakini anaweza kuamua kuukatisha kama atadhani uwepo wake kwenye kikosi hicho unamfanya kuwa na majanga tu.

TURIN, ITALIA . CRISTIANO Ronaldo wameshaanza kumvuruga huko Juventus, ambako Kocha Maurizio Sarri alimtoa kwenye mechi dhidi ya AC Milan, jambo lililomfanya supastaa huyo wa Kireno kuchukia sana na kuondoka uwanjani kabla mechi haijamalizika.

Baada ya kutolewa, Ronaldo, 34 aliamua kwenda moja kwa moja vyumbani na kisha kuwasha gari lake na kuondoka, wakati mechi ikiwa bado inaendelea.

Mchezaji aliyeingizwa kuchukua nafasi yake, Paulo Dybala, ndiye aliyekuja kufunga bao la ushindi kwa Juventus.

Kitendo hicho cha Ronaldo kiliwakera wachezaji wenzake kwamba anajiona yeye ni bora kuliko wengine. Jambo hilo linaweza kumfanya Ronaldo afungiwe miaka miwili kwa kuondoka uwanjani kabla ya mechi kumalizika, huku wachezaji wenzake wa Juventus wakitaka awaombe radhi.

Mkataba wa Ronaldo huko Turin unafika tamati 2022, lakini anaweza kuamua kuukatisha kama atadhani uwepo wake kwenye kikosi hicho unamfanya kuwa na majanga tu.

Kama Ronaldo ataamua kuondoka, basi huku ndiko anakoweza kwenda supastaa huyo mshindi mara tano wa Ballon d’Or.

Inter Miami

Kwa kubeba ubingwa mara tano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ronaldo anaweza kudhani kwamba imetesha, ameshaiteka Ulaya vya kutosha, hivyo ni wakati wa kwenda kwingineko na hapo, Marekani inaweza kuhusika.

Kinachoelezwa ni kwamba David Beckham amekuwa akiwapigia simu mastaa kibao akiwataka waende wakajiunge na timu yake ya Inter Miami inayotarajia kuanza kucheza kwenye MLS huko Marekani.

Anachokiamini Beckham ni kwamba kwa kuwa na mastaa kwenye kikosi chake basi kitavutia mashabiki wengi kwenda kuiona timu hiyo na huenda akampigia simu Ronaldo pia akatue kwenye chama lake kama akiona kwamba yupo tayari kuachana na Juventus.

Man United

Hili likitokea basi zitakuwa shangwe kubwa kwa Manchester United bila ya kujali kuhusu umri wa supastaa huyo wa Ureno. Ronaldo alicheza kwa mafanikio makubwa sana Old Trafford kabla ya kuondoka kwenda Real Madrid na kama watatambua anapatikana, bila ya shaka mabosi wa Man United watafanya kila wanaloweza kunasa saini yake.

Man United inatafuta mtu wa kuwafungia mabao na kama watadhani Ronaldo anapatikana, basi watakwenda mbio kunasa saini yake kwa sababu wanajua wazi huduma ya supastaa huyo inaweza kuwasaidia pia kuondokana na ukame wa kubeba taji la Ligi Kuu England. Mziki wa Ronaldo pekee yake ni balaa.

Real Madrid

Los Blancos wamekuwa kwenye wakati mgumu tangu Ronaldo alipoondoka kwenye kikosi hicho mwaka jana, ambapo aliongoza timu hiyo kubeba mataji manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ndani ya miaka mitano. Kwenye dirisha lililopita wamemsajili Eden Hazard, lakini ameshindwa kufanya kweli, huku Gareth Bale akiishia tu kuzomewa na mashabiki wa Bernabeu.

Bila ya shaka wakisikia kwamba Ronaldo anapatikana, Madrid watakwenda moja kwa moja kujaribu kuinasa saini ya mchezaji huyo ili arudi kukipiga kwenye kikosi chao, huku mabosi wa La Liga nao wakiamini ule mwamko umeshuka kutokana na staa huyo na hivyo kunakuwa hakuna ushindani wa Ronaldo na Lionel Messi uliozoeleka kwa miaka kibao.

PSG

Kutokana na Kylian Mbappe kuhusishwa na mpango wa kutua Juventus kwa Pauni 335 milioni, Paris Saint-Germain bila ya shaka watahitaji mchezaji wa kiwango bora wa kuja kuziba pengo la mchezaji huyo.

Na Ronaldo anaweza kuwa jibu sahihi kwenye hilo la kumbadili Mbappe kwenye kikosi cha PSG, lakini pia pengine atawaongoza vyema kwenye mikikimikiki ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, taji ambalo ndilo linalosakwa zaidi na timu hiyo tangu ilipoanza kuwa chini ya mabilionea wa Kiarabu.

Kila anakokwenda Ronaldo lazima aache alama zake na bila ya kujali umri wake wa sasa, huduma yake inaweza kuwa kitu muhimu zaidi kwa mabingwa hao wa Ufaransa.

China

Ronaldo anawezakuamua pia kwenda Mashariki ya Mbali ni chaguo bora la kwenda kustaafia huko. Klabu za China zitakuwa kwenye vita kali na kulipa kiwango chochote cha pesa kitakachotakiwa kama tu wanapata uhakika wa kwamba Ronaldo anapatikana na kwamba anaweza kwenda kucheza kwenye ligi yao.

Ukweli ni kwamba si jambo linaloshindikana kwamba Ronaldo kwenda kumalizia soka lake nje ya Bara la Ulaya na hilo likitokea, basi Asia au Amerika ni kitu kinachoonekana bayana kwenda kutokea kwenye maisha ya supastaa huyo wa Kireno kabla hajaamua