Nchimbi afunga bao baada ya siku 416

Tuesday April 20 2021
nchimbiii pic
By Thomas Ng'itu

WINGA Ditram Nchimbi wa Yanga ametoa gundula kutotupia wavuni baada ya kufunga bao la kuongoza katika mchezo wao dhidi ya Gwambina  unaoendelea katika uwanja wa Benjamin Mkapa leo usiku.

Nchimbi anakuwa amekata ukame wa mwaka mmoja, mwezi mmoja na siku 20 baada ya kukaa bila kuifungia bao lolote tili hiyo.

Katika mchezo huo Nchimbi alianza kwa kusuasua baada ya kupoteza mipira mingi hasa alipokosa umakini wa kupiga pasi.

Yanga walionekana kuhitaji zaidi bao la mapema  lakini mipango yao ilikuwa ikikwama kutokana na washambuliaji wake kukosa umakini.

Dakika saba Yacouba Sogne alipata nafasi lakini alikosa utulivu katika kumalizia na kupiga shuti ambalo liliguswa na mabeki wa Gwambina na kuondoa mpira huo.

Mabeki wa Gwambina wakiongozwa na Novatus Lufunga walikuwa hawawaruhusu washambuliaji wa Yanga, Yacouba Sogne na Deus Kaseke wasiingie kwenye boksi.

Advertisement

Dakika 18 Nchimbi alifyatuka shuti kali na kwenda moja kwa moja wavuni na kuibua shangwe uwanja mzima wa Benjamin Mkapa.

Licha ya Gwambina kutanguliwa  walikuwa wanapeleka mashambulizi kupitia kwa Rajab Athuman ambaye alikuwa na spidi ya kupeleka mashambulizi.

NABI JUKWAANI
Wakati Yanga ikiwa inaongoza kocha mpya wa Nasreddin Nabi alikuwa jukwaani akiufatilia mchezo huo.

Nabi ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu Yanga, alikuwa jukwaani pamoja na mabosi wa klabu hiyo wakifatilia mchezo.

Baada ya mapumziko kocha huyo alionekana kuzungumza mawili matatu na mabosi wa Yanga juu ya mchezo huo.

Advertisement