Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nafasi nyingine kwa Samatta

Muktasari:

Wapinzani wao hao langoni mwao anasimama  kipa mkongwe wa Ivory Coast, Aboubakar Barry.

MWANDISHI WETU

MBWANA Samatta leo Jumamosi anatarajiwa kushuka tena uwanjani wakati timu yake ya Genk itakapokuwa ugenini katika mfululizo wa mechi ya Ligi Kuu Ubelgiji.

Samatta amekuwa haanzishwi na kocha Peter Maes, badala yake aliingizwa dakika 15 za mwishoni katika mechi mbili zilizopita ambapo timu yake iliibuka kidedea.

Leo Jumamosi Genk inayoshika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi hiyo maarufu kwa jina la Jupiler League, itakuwa ugenini kuvaana na timu iliyo katika nafasi ya 12, Lokeren.

Wapinzani wao hao langoni mwao anasimama  kipa mkongwe wa Ivory Coast, Aboubakar Barry.

Timu hiyo pia ina mshambuliaji wa Kibrazili aitwaye Jaja (si yule wa zamani wa Yanga) ambaye katika mechi 14 ametupia mabao matatu.

Katika mechi mbili ambazo Samatta alizoingizwa kucheza dakika 15 za mwishoni, Genk iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mouscron Peruwelz na kuigagadua Waasland Beveren kwa mabao 6-1.

Samatta amekuwa akishukuru hata kupata hizo dakika chache kucheza kwa madai ni kama zinampa uzoefu wa kuizoea ligi hiyo kabla ya kuanza kufanya yake.

Mchezaji huyo anaamini baada ya muda si mrefu, kocha wake atakuwa akimwongezea muda wa kuwapo uwanjani.