Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nabi: Kwa silaha hizi mtakoma, amtaja Aziz Ki, Morrison

Nabi afunguka, Prisons wacheka

INGAWA Yanga hawajatangaza rasmi kumsajili winga Bernard Morrison, lakini habari za ndani na uhakika ni kuwa winga huyo ambaye msimu huu ameitumikia Simba yupo tayari kumwaga wino kwenye yake hiyo ya zamani kwa msimu ujao.

Wakati taarifa hizo zikiwepo pia Yanga imekamilisha usajili wa winga kutoka Asec Mimosas, Stephano Aziz Ki aliyekuwa akiwindwa na Simba.

Usajili wa mastaa hao ukikamilika wote basi utamka wigo mpana kocha Nassredine Nabi kuamua namna ya kuwatumia.

Nabi aliliambia Mwanaspoti anawapongeza viongozi wa timu hiyo kukamilisha usajili wa mchezaji bora na mwenye kipaji, Aziz Ki.

Alisema kama kikosi chake msimu ujao kitakuwa na Morrison na Ki maana yake wataongeza makali ya timu pamoja na uwezo mkubwa wa kufunga mabao zaidi ya wakati huu.

“Ukiangalia Morrison na Ki wote wanacheza nafasi zinazofanana kwa maana ya winga wa kushoto na kulia pamoja na nyuma ya mshambuliaji, ila matumizi yao yanaweza kuwa tofauti,” alisema Nabi.

“Wanaweza kuanza wote wawili kikosi cha kwanza kila mmoja akichezea kutokea pembeni kama winga kutokana na uwezo wao wa kufunga mabao, kutengeneza nafasi za kufunga na kuwasumbua mabeki wa timu pinzani, naamini watafanya vizuri.

“Naweza kuwatumia mmoja winga na mwingine akacheza nyuma ya mshambuliaji nalo ni sahihi. Matumizi ya tatu kwao mmoja anaweza kuanza mwingine akatokea benchi kisha akaingia kipindi cha pili kuongeza makali ya timu kama mwanzo wa mechi.

“Ni wazi kama uongozi utakuwa umekalisha usajili wa mchezaji aina ya Morrison ni mzuri na anaweza kufanya kazi kutokana na uwezo wake ulivyo, ila tusubiri muda ufike kila kitu kitakuwa wazi kwani sasa lipo kwa uongozi sio kwangu.”

Katika hatua nyingine, Nabi alisema msimu huu Yanga imekuwa na shida kwa mawinga Yacouba Sogne aliyeumia, Chicco Ushindi majeraha ya mara kwa mara, Dickson Ambundo na Denis Nkane hawakucheza mfululizo.

Alisema almtumia Saido Ntibazonkiza ambaye kiasili sio winga moja kwa moja kwani anaweza kucheza zaidi nyuma ya mshambuliaji wa kati. “Jesus Moloko alikuwa anacheza mfululizo baadaye alipata majeraha, ilikuwa shida kweli msimu huu eneo hilo kutokana na changamoto hizo mfululizo ndani ya timu,” alisema.

“Kama tutakuwa na Morrison na Ki msimu ujao maana yake tutakuwa tumepata tiba sahihi ya kile kilichokuwa shida.”