Nabi apewa rungu Yanga

Thursday June 10 2021
nabi pic
By Olipa Assa

KOCHA wa timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars, Bakari Shime amesema; “Ni kweli Yanga inahitaji kujiweka imara hasa kuelekea usajili ambao Nabi ataufanya, ni wachezaji gani ambao wataendana na mifumo yake ambayo kwasasa ni ngumu kuijua kwani alikuwa anawasoma wachezaji ili kumalizia msimu huu.”

Kwa mujibu wa Shime, Nasreddin Nabi bado hajaonyesha aliyonayo na anahitaji muda na asiingiliwe kwenye usajili.

Aliyewahi kuwa Katibu Mwenezi wa Yanga, Abdallah Sauko alisema inahitajika kuwa na kamati ya usajili sahihi itakayojitafakari katika sajili nne, imeshindwaje kuwapata wachezaji namba tisa na 10, pia alishauri Nabi atafutiwe kocha msaidizi mzawa.

“Tatizo Yanga halipo kwa makocha. Nashauri kocha aliyepo atafutiwe kocha mzawa imara wa kusaidiana naye, ndio maana inakuwa ngumu kumjaji kwani bado anaendelea kuwasoma wachezaji,”alisema Sauko.

Nabi alianza kuinoa timu hiyo, ikiwa inaongoza ligi kwa pointi 57 zilizokusanywa na makocha watatu kwa nyakati tofauti, ambapo kwasasa ina pointi 61 ipo nafasi ya pili, huku Simba ikikaa kileleni kwa alama 67.

Mechi za ligi ilizocheza chini ya kocha huyo ni dhidi ya Azam FC ambapo Yanga ilichapwa bao 1-0, ilishinda mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania na ilitoka suluhu na Namungo hivyo kujikusanyia pointi nne na aliivusha timu hiyo kutinga nusu fainali za ASFC baada ya kushinda mechi mbili.

Advertisement
Advertisement