Mwamuzi pambano la Mayweather vs McGregor atajwa
Marekani. Mwamuzi wa pambano la mabondia Floyd Mayweather na Conor McGregor linalotarajiwa kufanyika wiki ijayo, amewekwa hadharani jana Alhamisi.
Robert Byrd ndiye atakakuwa shuhuda kwenye Ukumbi wa T-Mobile Arena, Las Vegas nchini Marekani, huku Mayweather akitaka kuweka rekodi ya kutopigwa kwenye mapambano aliyoshiriki.
Pia iwapo Mayweather atafanikiwa kumshinda mpinzani wake, Conor McGregor litakuwa pambano la 50 kuibuka na ushindi.