Mwamuzi ang'atwa na nyoka uwanjani, taharuki yazuka

Muktasari:

  • Mashabiki walioshuhudia video hiyo katika mitandao ya kijamii walimsifia Gorcic kwa ujasiri wake wakishauri Uefa imchague awe mwamuzi wa fainali ya Ligi ya Mabingwa.

BELGRADE, SERBIA. Mchezo wa ligi ya madaraja ya chini Serbia kati ya GFS Leskovac Gornje Sinkovce na Radnik 2013, ulisimama kwa muda baada ya nyoka kuingia uwanjani na kumng'ata mwamuzi mara mbili.

Mchezo huo ulisimama na baadhi ya watu waliingia uwanjani kwa ajili ya kumtoa nyoka huyo, mmoja wao alionekana akiwa na begi akijaribu kumtega aingie lakini ilishindikana.

Picha za video zilimuonyesha mwamuzi, Aleksandar Gorcic, akiwa mtulivu wakati nyoka huyo akiwa anatembea na alimvizia kwa makini kisha akaenda kumshika na kumtupa nje ya uwanja.
Wakati anamshika baada ya kuwa amemkanyaga nyoka huyo huyo alifanikiwa kumng'ata mara mbili Gorcic.

Mashabiki walioshuhudia video hiyo katika mitandao ya kijamii walimsifia Gorcic kwa ujasiri wake wakishauri Uefa imchague awe mwamuzi wa fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Licha ya kung'atwa mwamuzi huyo anaendelea vizuri na hakuna madhara yoyote yaliyotokea.