Muumini kufunga mwaka Dodoma

BENDI ya Double M Plus chini ya Muumin Mwinjuma inatarajia kufanya onesho kubwa la kufunga mwaka Ukumbi wa 4 Ways Nkuhungu jijini Dodoma siku ya mkesha wa Mwaka Mpya.
Muumini amesema pamoja na kujiandaa kwa sherehe ya miaka 30 tangu aanze muziki, ameamua kufunga mwaka mjini Dodoma kwa lengo la kuendelea kutambulisha nyimbo zake ambazo zimo kwenye albamu yake ya 'Nimefulia'.
"Kwanza katika mikoa yote, Mkoa wa Dodoma umepata bahati ya kusikia nyimbo zangu ambazo zipo kwenye albamu yangu ninayotarajia kuzindua siku ya miaka 30 tangu nianze kuimba, nitapiga nyimbo zote kwa mara ya kwanza Dodoma, hii ni bahati kwa wakazi wa Dodoma na maeneo ya karibu, wajitokeze kuja kupata burudani hiyo" alisema Muumini
Muumin ambaye amewahi kupitia bendi kama Bantu Group, African Revolution 'WanaTamtam', Mchinga Sound 'Wana Kipepeo' Double M Sound, Mafahari Watatu, The African Stars 'Twanga Pepeta' na Victoria Sound amesema nyimbo zake za zamani kama Tunda, Maisha Kitendawili, Ndugu Lawama, Mgumba, Kilio cha Yatima, Mgumba part 2 na nyingine nyingi atazipiga siku hiyo ambapo kiingilio ni Sh 10,000.