Muda wowote Yanga kunatibuka

KUNA taarifa ya kwamba huko Jangwani mambo sio shwaari, inaelezwa kwamba kuna manung’uniko ya chinichini baina ya viongozi wa klabu hiyo kwenda kwa GSM.

Kwa kifupi GSM wamekuwa na nguvu kubwa Yanga kuliko viongozi kitu ambacho kimezua minong’ono hiyo ambayo inaelezwa kuitafuna klabu hiyo ndani kwa ndani.

Ndio maana imekuwa rahisi kwa mashabiki wa klabu hiyo kuwashambulia viongozi wao lakini sio GSM, wanaamini kuwa wawekezaji hao wamekuwa wakifanya kazi yao ipasavyo.

Kitendo cha mmoja wa viongozi wa GSM kuhusika moja kwa moja katika kuisaidia klabu hiyo kwa mambo mbalimbali inaeleza ni kitu ambacho baadhi ya viongozi wa klabu hawakifurahii kutokana na nafasi za upigaji kuzibwa tofauti na miaka ya nyuma.

Kila ambacho Yanga watahitaji kiongozi huyo wa GSM huwa mstari wa mbele kwa ufumbuzi, ukianzia usajili na hata malipo ya mishahara ya wachezaji.