Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtibwa yampigia hesabu Dante

Muktasari:

  • Kikosi hicho kinapiga hesabu nzito za kuongeza timu kwa ajili ya mashindano ya msimu ujao, huku ikigoma kuacha asili yake kwa kuwatumia vijana wengi inaowazalisha.

MTIBWA Sugar imerejea Ligi Kuu Bara, ikiwa na moto ikianza kupiga hesabu za maana kwa upande wa usajili ikisuka jeshi lake litakalowabakisha wasishuke.

Kikosi hicho kinapiga hesabu nzito za kuongeza timu kwa ajili ya mashindano ya msimu ujao, huku ikigoma kuacha asili yake kwa kuwatumia vijana wengi inaowazalisha.

Ndio maana kwa sasa inataka kumrudisha beki wa zamani Andrew Vincent ‘Dante’ kuja kuwaongezea nguvu.

Dante ambaye alikuwa Mtibwa baadaye akauzwa Yanga, amemaliza mkataba wake na KMC aliyoichezea ndani ya misimu Mitano mfululizo.

Baada ya mkataba wake kumalizika Dante amegoma kuongeza mkataba mwingine, huku akiwaambia mabosi wake kwamba anatafuta changamoto mpya.

Mwanaspoti linafahamu kuwa, beki huyo mkongwe tayari ameshaanza mazungumzo na mabosi wa Mtibwa ili kufanikisha usajili huo.

Taarifa kutoka ndani ya Mtibwa ilisema; “Tunataka kukiongezea nguvu kikosi chetu, tuna wachezaji wengi ambao hawana uzoefu na Ligi Kuu, kabla ya kushuka tulifanya makosa ya kuwa na timu yenye vijana wengi.

“Kuna wakongwe tutawaongeza ambao baadhi yao ni wale wanaoijua falsafa ya Mtibwa na wengine wenye guvu zaidi.”