Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtibwa mabingwa Championship, Cosmo yaifuata Biashara United First League

MTIBWA Pict

Muktasari:

  • Mtibwa iliyorejea Ligi Kuu Bara baada ya kushuka msimu uliopita, imeibuka mabingwa baada ya kuongoza msimamo na pointi 71, nyuma ya Mbeya City iliyomaliza ya pili na pointi 68, kufuatia ushindi wa 5-0, dhidi ya Green Warriors.

MTIBWA Sugar imeibuka mabingwa wa Ligi ya Championship kwa msimu wa 2024-2025, baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kiluvya United, huku Cosmopolitan ikiungana na 'Wanajeshi wa Mpakani', Biashara United kucheza First League msimu ujao.

Mtibwa iliyorejea Ligi Kuu Bara baada ya kushuka msimu uliopita, imeibuka mabingwa baada ya kuongoza msimamo na pointi 71, nyuma ya Mbeya City iliyomaliza ya pili na pointi 68, kufuatia ushindi wa 5-0, dhidi ya Green Warriors.

Licha ya Biashara kulazimishwa sare ya 2-2, leo dhidi ya Polisi Tanzania, ila kikosi hicho kilishuka daraja kikiwa na mechi mbili mkono, ambapo imeungana rasmi na Cosmopolitan iliyomaliza msimu kwa kuchapwa 2-1 na Songea United.

Timu nyingine zitakazowania 'play-off' ya kubaki Championship kwa msimu ujao, ni Transit Camp iliyomaliza nafasi ya 14 na pointi 21 baada ya kuchapwa mabao 3-2 na African Sports, iliyohitimisha msimu ikiwa ya 13 kufuatia kumaliza na pointi 22.

Kwa upande wa timu zitakazocheza 'play-off' ya kupanda Ligi Kuu Bara msimu ujao ni Stand United iliyomaliza ya tatu na pointi 61, ambayo itapambana na Geita Gold iliyojihakikishia mapema kumaliza nafasi ya nne baada ya kukusanya pointi 56.

Stand na Geita Gold zimemaliza msimu kwa sare ya bao 1-1, huku matokeo mengine yakishuhudia Mbuni ikiibuka na ushindi wa  3-2 dhidi ya Mbeya Kwanza, wakati TMA Stars ikiwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha iliifunga Bigman FC 2-1.