Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KenGold, Pamba Jiji mechi ya upande mmoja

KEN Pict

Muktasari:

  • Ken Gold imeshiriki Ligi Kuu msimu mmoja ambapo msimu ujao itacheza Championship baada ya kushuka daraja, huku Pamba Jiji ikiendeleza matumaini ya kukwepa aibu ya kushuka daraja.

WAKATI KenGold ikiikaribisha Pamba Jiji katika mwendelezo wa Ligi Kuu Jumanne hii, huenda mchezo huo ukawa wa upande mmoja kutokana na matokeo ya timu hizo, huku makocha wa timu hizo wakieleza matarajio yao.

Hadi sasa KenGold imeshuka daraja baada ya kushiriki msimu mmoja Ligi Kuu, huku Pamba Jiji ikiwa na matarajio ya kukwepa aibu ya kushuka daraja kutokana na matokeo iliyonayo kwa sasa.

Itaendelea pia kuwakosa baadhi ya nyota wake waliosimamishwa kwa madai ya utovu wa nidhamu ambao ni Seleman Bwenzi, James Msuva, Abdalah Masoud ‘Cabaye’ Steven Duah na kocha wa viungo, Uhuru Seleman.

Pamba Jiji iliyopanda Ligi Kuu msimu huu ipo nafasi ya 13 kwa pointi 27, ambapo inahitaji ushindi Jumanne hii ili kuendeleza matumaini ya kubaki salama kwenye mashindano hayo msimu ujao.

Kocha Mkuu wa KenGold, Omary Kapilima amesema pamoja na kwamba wameshuka tayari, lakini hawataingia kinyonge akieleza kuwa mchezo huo utakuwa ni wa kulinda heshima yao licha ya kilichowakuta.

Amesema kukosekana kwa baadhi ya wachezaji ambao bado tuhuma zao hazijafikia muafaka, waliopo kikosini wataweza kupambania nembo ya timu hiyo kuhakikisha wanashinda.

“Pamoja na kushuka daraja hatutakubali kupoteza kirahisi, tutapambana bila unyonge, tumekuwa na muda mwingi wa mazoezi na matarajio yetu ni kushinda mchezo huo japo hausaidia kwa chochote," amesema Kapilima.

Kocha Mkuu wa Pamba Jiji, Fred Felix ‘Minziro’ amesema baada ya kupoteza mechi iliyopita dhidi ya Simba kwa mabao 5-1, amekuwa karibu na wachezaji kuwaandaa kisaikolojia na kwamba mechi ya kesho ni muhimu sana kwao.

Amesema matokeo ya ushindi yatawaweka sehemu nzuri katika kukwepa kushuka daraja hata kucheza mchujo ‘play off’ akitamba kuwa anaamini kwa maandalizi waliyofanya watashinda mechi hiyo.

“Tunajua tunacheza na timu iliyoshuka lakini si kwamba tutadharau kwa namna yoyote badala yake ni kuingia kwa tahadhari kuhakikisha tunapata pointi tatu zitakazotuweka mazingira mazuri,” amesema Minziro.