Mshery aweka rekodi CAF

Mshery aweka rekodi CAF

NDIO. Golikipa wa Yanga Abutwalib Mshery, leo ameweka rekodi ya kucheza mechi ya kwanza ya kimataifa  kwa ngazi ya klabu akianza kwenye mechi dhidi ya Zalan FC ya Sudan Kusini, katika Ligi ya Mabingwa.

Mshery ndio amesimama kwenye milingoti mitatu akichukua nafasi ya Djigui Diarra ambaye hayupo kabisa kwenye kikosi leo.

Katika historia yake ya soka hii ndio itakuwa mara yake ya kwanza kucheza mechi ya kimataifa ya michuano ya CAF kwa ngazi ya klabu.

Kwa msimu huu hii inakuwa ni mechi ya pili kwa Mshery, baada ya kufanya hivyo pia kwenye mechi dhidi ya Coastal Union ambayo iliyomalizika  kwa Yanga kushinda mabao 2-0.

Kikosi cha Yanga kilichoanza leo golikipa ni, Abdutwalib Mshery mabeki, Djuma Shaban, Kibwana Shomari, Bakari Mwamnyeto, viungo Yannick Bangala, Khalid Aucho, Feisal Salum, Dickson Ambundo, washambuliaji Fiston Mayele, Aziz Ki, Jesus Moloko.