Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mpeni tu!: Okwi mpango mzima lakini kwa Zahera, Aussems nako moto

Muktasari:

  • Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi huenda ipo nafasi kubwa ya kuibuka mchezaji bora wa mwezi Oktoba kutokana na kiwango bora alichokionyesha. Okwi amefunga mabao saba katika mwezi huo na Simba ikajikusanyia pointi 12, ikiwa ni moja ya timu tatu zilizokusanya alama nyingine ndani ya mwezi huo ikilingana na Yanga, huku vinara wakiwa ni Azam iliyovuna pointi 15 za mechi zao tano.

USIBISHE. Emmanuel Okwi ndiye atakayenyakua tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Bara kwa mwezi Oktoba. Hii ni kwa sababu siku zote namba huwa hazidanganyi hata kidogo.

Mabao saba yaliyofungwa na raia huyo wa Uganda ndani ya mwezi huo yamemweka katika nafasi nzuri ya kunyakua tuzo hiyo akifuata nyayo za nyota wengine waliobeba tuzo hiyo akianza Meddie Kagere wa Simba aliyebeba ya Agosti na Eliud Ambokile wa Mbeya City aliyenyakua ile ya Septemba.

Mwanaspoti linaamini labda itokee miujiza tu, straika huyo aliyekuwa kinara wa mabao wa Ligi Kuu msimu uliopita kwa kutupia kambani mabao 20, vinginevyo Okwi atabeba tuzo hiyo, kutokana na uteuzi wa nyota wa mwezi kubebwa zaidi na ufungaji mabao na kuibeba timu yake ndani ya mwezi husika.

Katika mechi nne ambazo Simba ilicheza Oktoba na Okwi kufunga mabao hayo saba, ilikusanya pointi 12, ikiwa ni moja ya timu tatu zilizokusanya alama nyingine ndani ya mwezi huo ikilingana na Yanga, huku vinara wakiwa ni Azam iliyovuna pointi 15 za mechi zao tano.

Okwi alifunga mabao yake katika mechi dhidi ya African Lyon, Simba ikishinda mabao 2-1 yeye akifunga moja, kisha akafanya hivyo tena dhidi ya Stand United, wakati Chama la Wana wakifa kwa mabao 3-0.

Akafunga mawili wakati wakiizamisha Alliance kwa mabao 5-1 kabla ya kufunga kazi wakati Simba ikiipapasa kibabe Ruvu Shooting kwa mabao 5-0, yeye akitupia matatu (hat trick).

Nyota anayemfuatia kwa mabao ndani ya mwezi huo ni kinara wa orodha ya Wafungaji mpaka sasa katika Ligi Kuu, Eliud Ambokile aliyefunga mabao manne katika mechi nne ilizocheza timu yake ya Mbeya City ambayo ilikusanya pointi 11.

Ambokile alifunga mawili katika mechi ya ugenini dhidi ya Stand United, wakati City ikishinda 2-0, kabla ya kufunga bao pekee walipoilaza Mwadui jijini Mbeya na kuhitimisha katika mechi ya sare ya 2-2 dhidi ya Mbao FC iliyopigwa Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

MECHI 49 ZA KIBABE

Kama hujui tu ndani ya Oktoba zilichezwa jumla ya mechi 49 zilizozalisha mabao 88, ambapo mbali na Okwi na Ambokile waliotupia mabao mengi, wachezaji wawili, Said Dilunga wa Ruvu Shooting na Yahya Zayd wa Azam FC walifuata wakiwa na mabao matatu kila mmoja.

James Msuva aliyehitimisha mabao ya mwisho ya Oktoba wakati timu yake ya KMC ikiichapa Ndanda kwa mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa Oktoba 31, aliingia orodha ya waliofunga mabao mawili ndani ya mwezi huo akiwa pamoja na Eliuter Mpepo wa Singida Utd na Ibrahim Ajibu wa Yanga anayeongoza kwa kuhusika na mabao 11 kati ya 16 ya timu yake hadi sasa.

Wengine waliofunga mabao mawili kila mmoja ni; Habib Kiyombo (Singida Utd), Ibrahim Irakoze Nasser (Mwadui), Donald Ngoma (Azam), Deo Anthony (Coastal Union), Said Khamis (Mbao), Abdulrahman Mussa (JKT TZ), Zawadi Mauya (Lipuli), Evarigestus Mujwahuki (Mbao), Vitalis Mayanga (Ndanda), Jacob Massawe (Stand Utd), Adam Salamba na Cletus Chama (wote wa Simba), Jerome Lambele (Biashara Utd) na Issa Rashid (Lipuli).

Huku Mkongoman Heritier Makambo, Rafael Daud, Feisal Salum na Mrisho Ngassa wa Yanga pamoja na Shiza Kichuya, Meddie Kagere na Asante Kwasi wa Simba wakitengeneza orodha ya wachezaji 37 waliofunga bao mojamoja ndani ya Oktoba uliohitimishwa Oktoba 31.

VITA YA ZAHERA, PLUIJM NA AUSEMMS

Katika kinyang’anyilo cha tuzo hiyo kwa upande wa makocha ni Mwinyi Zahera, Patrick Ausemms na Hans Pluijm ambao wote kwa pamoja waliziongoza timu zao kupata ushindi.

Mwezi Agosti tuzo hiyo ilikwenda kwa kocha wa Mbao FC, Amri Said. Septemba ni Zahera ameiongoza timu yake katika michezo minne na kufanikiwa kuibuka na ushindi katika michezo yote bila kuruhusu bao hata moja na yeye kuambulia pointi 12 na mabao 7

Wakati wapinzani wake ni Pluijm ambaye ameiongoza Azam kucheza michezo mitano na kushinda yote na kuambulia pointi 15 na kufanikiwa kufunga mabao saba na kuruhusu moja.

Kwa upande wa kocha wa Simba, Ausemms ameiongoza timu yake kucheza michezo minne na kufanikiwa kushinda yote na kuambulia pointi 12 huku ikifunga mabao 15 na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara mbili.