Morris: Tumefuzu ila ushindani ulikuwa mkubwa

Sunday February 28 2021
moris azam
By Thomas Ng'itu

NAHODHA wa Azam FC, Agrey Morris amesema katika mchezo wao wa mtoano wa Kombe la Shirikisho la Azam  dhidi ya Mbuni ulikuwa ni mchezo mgumu kwa timu zote.

Katika mchezo huo Azam iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Prince Dube dakika 45+ baada ya kuwachambua mabeki wa Mbuni na kufunga kwa shuti la chini chini.

azam pic

Morris alisema katika mchezo huo hakuna kingine walichokuwa wanahitaji zaidi ya ushindi hivyo kusonga mbele kwao ndio muhimu.

"Mchezo ulikuwa mgumu na kila timu ilikuwa ikihitaji matokeo, muhimu ni kusonga mbele katika mashindano haya".

Aliongeza kwa kusema "Baada ya kupata goli tuliona tusizidi kushambulia sana, wenzetu wanaweza wakapiga kaunta halafu wakasawazisha".

Advertisement
Advertisement