Molinga apiga mbili za fasta, Yanga ikisawazisha

Muktasari:

Molinga amejiunga Yanga kwa mkopo kwenye usajili wa dirisha kubwa msimu huu akitokea AC Lega ya DR Congo.

Dar es Salaam.Mshambuliaji David Molinga amegeuka 'lulu' baada ya kupiga mabao mawili ya haraka na kuisawazishia Yanga matokeo kuwa 3-3 katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Polisi Tanzania unaoendelea kwenye Uwanja wa Uhuru Leo Alhamisi.

Molinga hakuanza vizuri dakika 45 za mwanzo alirejea kwa kishindo na kuwapa nguvu mashabiki wa Yanga waliokuwa nyuma kwa mabao 3-1 hadi dakika ya 64.

Dakika ya 65 na 68, Molinga alipachika mabao ya fasta na kuisawazishia Yanga katika mchezo huo.

Hayo ni mabao ya kwanza kwa Molinga kufunga kwenye Ligi kuu, moja akifunga kwa faulo na jingine kwa shuti la nje ya kumi na nane lililodakiwa ndani na kipa wa Polisi Tanzania.