Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mo Dewji atoa neno paredi la ubingwa Simba

MO DEWJI Pict

Muktasari:

  • Bosi huyo ametoa kauli hiyo leo kwa njia ya simu wakati wa kilele cha paredi ya ubingwa kilichofanyika Coco Beach, Dar es Salaam, ambapo maelfu ya mashabiki wa Simba walikusanyika kusherehekea taji hilo.

RAIS wa Heshima wa Simba na mwekezaji wa klabu hiyo, Mohamed Dewji 'Mo', amesema mafanikio ya kutwaa Kombe la CRDB yanapaswa kuwa chachu ya kuipeleka timu hiyo kwenye mafanikio makubwa zaidi.

Mo ameeleza kuwa ndoto yake kubwa ni kuona Wekundu wa Msimbazi wakitwaa ubingwa wa Afrika.

Bosi huyo ametoa kauli hiyo leo kwa njia ya simu wakati wa kilele cha paredi ya ubingwa kilichofanyika Coco Beach, Dar es Salaam, ambapo maelfu ya mashabiki wa Simba walikusanyika kusherehekea taji hilo.

Akizungumza na mashabiki, Mo ameanza kwa kuwapongeza wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na wanachama kwa mchango wao uliowezesha Simba kumaliza msimu ikiwa na kombe.

"Nawapongeza sana mashabiki wa Simba, nawapongeza viongozi, nawapongeza wachezaji na kila Mwanasimba kwa mafanikio haya. Asanteni kwa kuendelea kuiunga mkono timu yetu," amesema.

Mo amesema ataendelea kujitolea na kuwekeza ndani ya Simba ili kuhakikisha klabu hiyo inazidi kukua na kushindana katika viwango vya juu zaidi barani Afrika.

Mwekezaji huyo amesema, pamoja na kufurahia Kombe la CRDB, kiu yake kubwa sasa ni kuona Simba ikifanikiwa kutwaa taji la Afrika iwe Ligi ya Mabingwa au Kombe la Shirikisho Afrika.

Kauli hiyo imepokewa kwa shangwe na maelfu ya mashabiki waliokuwa Coco Beach huku wakipaza sauti za kuunga mkono azma hiyo.

Mo amehitimisha salamu zake kwa kuwaombea kila la heri Wanasimba, akisisitiza kuwa kwa umoja na mshikamano klabu hiyo inaweza kufikia malengo makubwa zaidi  misimu ijayo.