Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kapombe aahidi mataji zaidi msimu ujao

KAPOMBE Pict

Muktasari:

  • Kapombe amesema kwa niaba ya kikosi kizima cha Simba, wachezaji wanathamini mapokezi makubwa waliyopewa tangu walipowasili Dar es Salaam hadi kufikia hitimisho la paredi hiyo Coco Beach.

NAHODHA wa Simba, Shomary Kapombe amewashukuru mashabiki wa klabu hiyo kwa kujitokeza kwa wingi leo Jumapili katika paredi ya ubingwa wa Kombe la Shirikisho la CRDB, huku akisema sapoti hiyo ikiendelea, msimu ujao watafanya vizuri zaidi.

Kapombe amesema kwa niaba ya kikosi kizima cha Simba, wachezaji wanathamini mapokezi makubwa waliyopewa tangu walipowasili Dar es Salaam hadi kufikia hitimisho la paredi hiyo Coco Beach.

"Kwa niaba ya wachezaji, kwanza napenda kuwashukuru mashabiki na wanachama wote ambao mmejitokeza kwa wingi. Hatukutarajia kuona umati mkubwa kama huu. Asanteni sana kwa kutuunga mkono," amesema Kapombe.

Nahodha huyo amesema paredi ya Simba imeweka rekodi kwa muda mrefu wa kusherehekea, akieleza kuwa msafara huo ulidumu kwa takribani saa 10.

"Paredi yetu imetumia saa 10 na bado watu wanaendelea kushangilia. Hii inaonyesha namna ambavyo mnaipenda Simba na mnavyothamini mafanikio ya timu yenu," amesema.

Kapombe amekiri kuwa Simba haikuanza vizuri msimu huu lakini juhudi za wachezaji, benchi la ufundi na uungwaji mkono wa mashabiki umeiwezesha timu kumaliza kwa kutwaa Kombe la CRDB.

"Msimu hatukuanza vizuri, lakini tumemaliza vizuri. Hilo limetokana na ushirikiano wa kila mmoja ndani na nje ya uwanja," amesema.

Nahodha huyo amewaomba mashabiki kuendelea kuipa timu sapoti kama walivyoonyesha katika paredi hiyo, akisisitiza Simba ina malengo makubwa zaidi katika msimu ujao.

"Tunaomba jambo moja, kama mlivyokuwa nasi leo, msimu ujao muendelee kutusapoti kwa nguvu hizi hizi. Tukipata sapoti kama hii tunaamini tutafanya makubwa zaidi kuliko tuliyofanya msimu huu," amesema mkongwe huyo ambaye yupo klabuni hapo tangu 2017.